Papa:Katika Basilika ya Familia Takatifu wanahija wapokelewe kwa sala!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika hotuba ya Baba Mtakatifu alipoktana mjinimVatican Jumamosi tarehe 17 Februari 2024 na Wawakilishi wa Bodi ya Ujenzi ya Kanisa kuu la Familia Takatifu ya mji wa Barcelona nchini Hispania amefurahi kukutana nao wakiwa na familia zao ambapo amesema kama alivyorudia mara nyingi katika fursa ya mwaka wa sala wa kujiandalia Mwaka wa Jubilei 2025 kuwa mwaka mzima ni katika maombi kwa ajili ya hiyo. Ni muhimu kwamba hali halisi ya maombi isipotee kwenye mahekalu, lazima iwe moja ya vipaumbele kwa wale, kama wao, ambao wamepokea jukumu la kutunza mahekalu.
Kwa hakika Papa amesema wao wameona kwamba Basilika ya Familia ya Sagrada imeundwa ili kila ukumbi uwe na mada, inayooneshwa na vifungu vya Maandiko na kuandaliwa kwa maombi. Hivyo mlango wa kwanza, ni ule wa imani, nyuma ya sura ya Yesu akiwahubiria madaktari, unatuonesha Utatu Mtakatifu. Imani inayohubiriwa lazima iwe maombi. Kila mara.
Mlango wa kati wa upendo, ambao sura yake kuu hasa ni ile ya Familia Takatifu, inatualika kuinua mitazamo yetu kuelekea fumbo la Umwilisho na kutoka hapo tuchambue shanga za rozari inayoshuka kando ya madirisha, tukitengeneza nyota ya Bethlehemu, karibu kama kusema: “hapa kuna nuru yetu.” Na ni hasa katika kuabudu, katika sala ya kutafakari ya mafumbo, kwamba tunajifungua wenyewe katika mwanga huo, kama dirisha kubwa la hekalu lao.
Kwa hivyo Baba Mtakatifu Francisko amewaalika kuwakaribisha mahujaji wanaokaribia kwenye Basilika, ili kuwatambulisha kwa mtazamo wa sala kutafakari mpango wa picha ya mtumishi wa Mungu Antoni Gaudí katika ukamilifu, ili kwamba kama vile vilele na minara ya kengele, mitazamo yao iinuliwe juu na sauti zao zitangaze pamoja na Malaika: “Mtakatifu, Mungu wetu hafi.” Asante kwa kila kitu unachofanya, asante. Mungu awabariki.