Ratiba za mikutano ya Papa imeharishwa kwa sababu ya mafua
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilisasisha asubuhi ya Jumatatu tarehe 26 Februari 2024 kuhusu uamuzi wa Papa wa kusitisha vikao vilivyokuwa vimepangwa “kama tahadhari”, kama ilivyokuwa pia Jumamosi tarehe 24 Februari iliyopita, wakati ilipotolewa taarifa ya kuwa Papa Francisko alikuwa na homa, japokuwa siku ya Jumatatu wamebainisha kwamba ni “Dalili za mafua kidogo” ambazo haziambatani na homa.
Katika sala ya Malaika wa Bwana
Hata hivyo licha ya udhaifu huo, Domenika tarehe 25 Februari ulimruhusu Papa Francisko kuweza kuchungulia dirishanai na kutoa tafakari yake na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Na mara baada ya sala hiyo, Askofu wa Roma aligusia juu ya miaka miwili tangu kuzuka kwa vita nchini Ukraine na kurejea kutoa miito ya kusitisha vita huko Palestina na Israel na pia kuzungumzia juu ya utekaji nyara nchini Nigeria na vurugu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia ahakusahau kuwakumbuka watu wa Mongolia wanaoteseka kwa baridi sana, huku akisisitizia juu ya mgogoro wa Tabianchi.