Tafuta

2024.03.11 Papa alikutana na Maaskofu wa Mkoa wa Marche Italia wakiwa katika ziara yao ya Kitume (Visita "ad Limina Apostolorum"). 2024.03.11 Papa alikutana na Maaskofu wa Mkoa wa Marche Italia wakiwa katika ziara yao ya Kitume (Visita "ad Limina Apostolorum").  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Maaskofu wa Marche:Papa yuko karibu na matatizo halisi ya maisha yetu!

Takriban saa 2 za mazungumzo ya moja kwa moja,na maswali na majibu juu ya changamoto mpya zinazongojea Kanisa katika mkoa wa Marche pia baada ya tetemeko la ardhi,janga la uviko na mafuriko.Hii ilikuwa wakati wa ziara ya Kitume (Visita ad limina)ya maaskofu wa Italia ya kati iliyofanyika tarehe 11 Machi 2024.Ambapo Rais wa Baraza la Maaskofu Marconi alisema:“Maneno ya kweli na ya dhati kutoka kwa Baba Mtakatifu akizungumza na waandishi wa Vatican News, mara baada ya mkutano huo.

Vatican News

Maneno ya dhati, ya ukweli, ya moja kwa moja, kutoka kwa mtu aliye karibu na shida halisi za maisha yetu ndivyo alisema Askofu  Nazzareno Marconi, rais wa Baraza la Maaskofu wa Marche, kwa waandishi wa Vatican News katika mazungumzo  ya tarehe 11 Machi 2024 mara baada ya kukutana na Baba Mtakatifu wakiwa katika ziara ya Kitume (Visita ad Limina). Takriban saa mbili za mazungumzo hasa ​​ya upole ambapo Papa, aliuliza kila mtu kujitambulisha na kuorodhesha changamoto na matatizo ya majimbo yao  binafsi.”

 

Papa kuonesha mshakamani na hali za majimbo

Kwa mujibu wa Askofu Marconi alibainisha kuwa, Papa  hasa alionesha mshikamano kwa hali ambayo majimbo yetu yanapitia kutokana na tetemeko la ardhi, mafuriko ... Hali zilizozidi wakati wa Uviko 19 na  kwamba sehemu nzuri ya mazungumzo ililenga “changamoto za kichungaji za wakati huu wa mabadiliko makubwa, hasa ukaribu wa familia na vijana na ugumu wa kusambaza imani kati ya vizazi.” Maneno pia alisisitiza katika taarifa iliyotolewa baada ya kusikilizwa na Baraza la Maaskofu wa Marche kuwa “Papa Francisko alijibu maswali, kuhimiza njia ya pamoja ya Makanisa ya Marche, kuonesha mshikamano na matatizo yetu, hasa nyenzo tata na zaidi ya yote ujenzi wa kijamii baada ya tetemeko la ardhi, janga na mafuriko. Papa, alithibitisha maaskofu katika ufahamu wao wa kazi ngumu ya kulivusha Kanisa la mkoa wa Marche kutoka katika mapokeo ya zamani na imani iliyopatikana zaidi ya yote katika parokia ndogo hadi siku zijazo tofauti.”

Ziara ya Kitume ya Maaskofu wa Marche
12 March 2024, 18:11