Tafuta

Bikira Maria wa Lourdes. Bikira Maria wa Lourdes. 

Ujumbe wa Papa kwa wanajeshi huko Lourdes:Huduma ya amani katika giza la kihistoria!

Katika fursa ya hija ya 64 Kimataifa mahali Patakatifu,Lourdes,Ufaransa kwa kundi la maaskari,Baba Mtakatifu alituma ujumbe uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican katika afla iliyoongozwa na Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa na mashirika ya Kimataifa:Shuhudia Injili kati yenu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Imekuwa ni utamaduni ambao ulianza miaka 64 iliyopita na kila wakati ni wa kusisimua kwa kile  ambacho kinaibua mwonekano wa maelfu ya sare mbalimbali zilizopangwa kwenye sala mbele ya Grotto ya Massabielle huko Lourdes nchini Ufaransa. "Kwa askari anayechagua kupiga magoti wakati wa maisha yake mbele ya Mama Yetu wa Lourdes, kwa wito wa kijeshi ni wazi ambapo popote  mnapotumwa toeni ushuhuda wa Injili kati yenu!" Ndivyo Baba Mtakatifu ameandika Ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin,  Katibu wa Vatican,  wakati wa afla ya hija ya kila mwaka ya kimataifa kwa maaskari katika Mahali Patakatifu Lourdes nchini Ufaransa, inayoongozwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Hija ya Lourdes mara zote ni ya ajabu na nzuri
Hija ya Lourdes mara zote ni ya ajabu na nzuri

Kama Bernadette ambaye alihimizwa na Bikira kuwaombea mapadre wamjengee Kanisa la ibada ili kuwaruhusu watu kuja katika maandamano, vivyo hivyo Papa Francisko amewaalika Askari hao: “waanze safari pia kiroho, kwanza kabisa kwa Mungu, lakini pia kwa kaka na dada zetu, ili kujenga ulimwengu unaounga mkono na wa kidugu.”

Ahadi ina nguvu kwa ajili ya huduma ya amani duniani

Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anaonesha juu ya “ahadi ambayo ina nguvu zaidi kwa sababu inawalenga wale ambao wanaitwa kuchukua nafasi isiyoweza kubadilishwa kwa manufaa ya wote na huduma ya amani duniani.” Hata kwa wale wanaovaa sare, Papa Francisko amebainisha kuwa “hija ni uzoefu wa imani unaotuwezesha kugundua uzuri wa kutembea pamoja, kusaidiana na kufikia wengine. “

Madhabahu ya Kimataifa Lourdes
Madhabahu ya Kimataifa Lourdes

Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha kuwa: “hija inakuruhusu kuwa karibu na wenzenu wagonjwa na waliojeruhiwa mikononi na kuwatunza na kuleta huruma ya Mungu kwa ulimwengu wa kijeshi.” Ulimwengu, unawahitaji, hasa katika wakati huu wa giza katika historia yetu. Tunahitaji wanaume na wanawake wa imani wenye uwezo wa kuweka silaha zao chini ili kuwa katika huduma ya amani na udugu.” Alihitimisha ujumbe wake.

UJUMBE WA PAPA KWA ASKARI HUKO LOURDES
25 May 2024, 11:23