Papa awaandikia vijana wa Romania:tumieni mitandao ya kijamii na sambazeni maadili
Vatican News
“Kuweni wabeba matumaini na wajenzi wa madaraja, mkitumia kila chombo kinachopatikana ili kupanda wema na upendo ulimwenguni.” Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliwaandikia vijana wa Romania wa jimbo la Iasi, akijibu barua yao iliyotumwa katikati ya mwezi Mei mwaka huu kupitia kwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ambaye alishiriki katika mkutano wa vijana wa Jimbo huko Iasi mnamo tarehe 18 na 19 Mei 2024 ulioandaliwa na Askofu Iosif Păuleț.
Tumieni mitando ya kijamii kwa ujasiri na ubunifu mkisambaza maadili
Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu aliwahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii “kwa ujasiri na ubunifu, kusambaza maadili ambayo yanajenga: urafiki, amani, mazungumzo kati ya makabila na tamaduni, familia na maadili ya Kikristo.” Na aliwasihi wajilinde dhidi ya kuwa watumwa wa simu za mikononi na kutoka katika kukwama kwa kujitenga katika maisha ya kawaida, kwa madhara ya maisha yao ya kweli.
Utajiri wa kweli upo katika mahusiano ya moja kwa moja na ya dhati
“Nendeni ulimwenguni, kutana na watu, sikilizeni historia zao, tazameni kaka na dada zenu machoni. Utajiri wa kweli upo katika uhusiano wa kibinadamu unaopatikana kila siku, kwa mawasiliano ya moja kwa moja na ya dhati,” alibainisha Papa. Na zaidi ya hayo Baba Mtakatifu aliwaalika kushiriki katika mkutano wa vijana wa kitaifa, utakaofanyika mwezi Septemba katika Jimbo la Brasov. “Itakuwa fursa ya thamani kukua pamoja katika imani, kushiriki uzoefu na kuimarisha njia zenu katika Kikristo.” Na hatimaye aliandika Papa Francisko kuwa “Msisahau kuniombea,” kwani Msaada wenu wa kiroho ni zawadi isiyokadirika ambayo inanisaidia kutumikia Kanisa na ubinadamu.”