Tafuta

Papa:Trieste ni bandari wazi,msimamo,ukarimu na utambuzi!

Papa Francisko,Dominika Julai 7 Julai akiwa huko Trieste katika hitimisho la Juma la 50 la Kijanii kwa Wakatoliki wa Italia mara baada ya misa na kusikiliza shukrani kutoka kwa Askofu wa Trieste amewatia moyo:"Mna kadi ya utambulisho ambayo ni dira.Kama wakristo tuna Injili inayotupatia maana ya matumaini."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Misa Takatifu na salamu kutoka kwa Askofu wa Jimbo la Trieste katika Uwanja wa Muungano wa Italia, Dominika tarehe 7 Julai 2024, akiwa huko kwa ajili ya kufunga Juma la toleo la  50 la Mafundisho Jamii ya Kikatoliki nchini Italia na kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, alianza kusema: “Kabla ya baraka ya mwisho ninapenda kuwasalimu ninyi nyote mliokusanyika katika Uwanja huu mzuri. Ninamshukuru Askofu kwa maneno yake na hasa kwa ajili ya maandalizi ya ziara yangu, na wale ambao kwa namna nyingi wameshirikiana hasa kwa ajili ya liturujia na kwa huduma mbalimbali: na kama ilivyo kwa  watu wengi walioshiriki kwa sala."Papa  Francisko kwa hiyo kwa wote hao amewahakikishia ukaribu wake: “wagonjwa na wafungwa, wahamiaji na kwa wote ambao wanapata ugumu wa maisha."

Misa ta Trueste
Misa ta Trueste

Papa akiendelea amesema: “Trieste ni moja ya mji ambao una miito ya kufanya waingie watu tofauti: awali ya yote kwa sababu ni bandari na bandari muhimu na kisha kwa sababu inajikuta njia panda kati ya Italia, Ulaya ya Kati na Nchi za Balkan. Katika hali hizo, changamoto kwa jumuiya ya kikanisa na kwa zile za kiraia ni kujua namna ya kuunganisha uwazi na msimamo, makaribisho na utambuzi.”

Misa kwa waamini Trieste
Misa kwa waamini Trieste

Papa Francisko kisha amebainisha kuwa imemjia akilini kusema: “mna kadi za kanuni” ili kukubiliana na changamoto hiyo! Kama wakristo tuna Injili ambayo inatoa maana na matumaini katika maisha yetu; na kama raia mnayo Katiba na “dira” inayaoaminika ili kutembea katika demokrasia." Kwa njia hiyo Papa amewatia moyo wa "kuendelea mbele bila kuogopa, wakiwa wazi, na msimamo thabiti katika thamani za kibinadamu na kikristo, huku wakikaribisha lakini bila kuathiri utu wa binadamu."

Papa Francisko huko Trieste
Papa Francisko huko Trieste

Na kutoka katika mji  huo wa kupyaishwa kwa jitahada zao,  ni ombo la Papa ili  kusali na kutenda kwa ajili ya amani; hasa kwa ajili ya nchi ya Ukraine inayoteseka, kwa ajili ya Palestina na Israeli, kwa ajili ya Sudan, Myanmar na kila watu ambao wanateseka kwa vita.” Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amesema “ Tumuombe kwa maombezi ya Bikira Maria anayefanyiwa ibada juu ya Mlima Grisa kama Mama na Malkia.”  Na baadaye walisali sala ya Malaika wa Bwana kabla ya kurudi jijini Vatican ambapo ulikuwa ndiyo mwisho wa hitimisho la Toleo la 50 la Mafundisho ya Kijamii Katoliki nchini Italia lililofunguliwa tarehe 3 Julai na mgeni Rasmi Rais wa Nchi Bwana Sergio Mattarella.

Mara baada ya Misa huko Trieste Papa ametoa shukrani
07 July 2024, 12:12