2024.09.04 Mkutano wa Papa  na maaskofu 2024.09.04 Mkutano wa Papa na maaskofu   (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Tahariri

Kile kinachopeleka Ulimwengu mbele ni Upendo wa Huruma!

Papa Francisko alieleza kuwa huruma“inakufanya uone mambo vizuri”

Andrea Tornielli

Kile kinachopeleka mbele ulimwengu nini? Wengine wanaweza kujibu uchumi, wengine mapambano ya nafasi, wengine udadisi, au hamu ya kufanya na kujaribu na wengine pia upendo. Zaidi ya miaka thelathini iliyopita huko nchini Argentina bibi mzee alimwambia Askofu Bergoglio kwamba huruma ya Mungu ni kizingiti kichoshikilia Ulimwengu(“ikiwa Bwana hangesamehe kila kitu, ulimwengu husingekuwepo”); leo hii, Papa Francisko alielekeza ni “injini" gani inayofanya Ulimwengu uende mbele.

Kutoka katika Kanisa Kuu la Jakarta, Papa alieleza kuwa kinachofanya Dunia iende  mbele  ni “Upendo unaotolewa” kwa huruma. Papa alisema kuwa huruma haijumuishi kutoa msaada au usaidizi kwa wahitaji “kwa kuwatazama kutoka juu hadi chini, kwa maana ya kuwadharau,” bali ina maana ya kuinama ili kweli kukutana na walio chini na hivyo kuwainua na kuwapa matumaini tena. Inamaanisha pia kukumbatia ndoto na matamanio ya ukombozi na haki kwa wahitaji, kuwa wahamasishaji na washirika nao."


Kuna wale wanaoogopa huruma, Mrithi wa Petro alisisitiza zaidi, “kwa sababu wanaona kuwa ni udhaifu” na “badala yake hujitukuza, kana kwamba ni fadhila, ujanja  wa wale wanaoangalia maslahi yao wenyewe kwa kujiweka mbali kwa kila mtu, kutojiruhusu “kuguswa” na chochote au mtu yeyote, hivyo kufikiria kuwa waangalifu zaidi na kuwa huru katika kufikia malengo yao binafasi.” Papa alifafanua zaidi kuwa: “lakini hii ​​ni njia ya uongo ya kutazama ukweli.” Kwa sababu “kinachofanya ulimwengu uendelee sio hesabu za maslahi,  ambazo kwa ujumla huishia kuharibu uumbaji na kugawanya jumuiya,  lakini ni upendo unaotolewa.

Huruma haifichi maono halisi ya maisha, kinyume chake, inatufanya tuone mambo vizuri zaidi, kwa nuru ya upendo.” Kwa njia hiyo ni huruma ambayo Yesu anatushuhudia katika kila ukurasa wa Injili: yeye habaki kutojali ukweli, anaguswa mtazamo wa macho, anajiruhusu kuumizwa na majanga na hitaji la wale anaokutana nao. Kinyume chake, kutojali, ambako kwa muda mrefu kumegeuka kuwa wasiwasi, hutufanya tuamini kuwa tuko huru zaidi lakini kiukweli hutufanya, kidogo kidogo kutokuwa  wa kibinadamu.”

Ufupisho wa Siku ya Papa tarehe 4 Septemba huko Jacarta, Indonesia
05 September 2024, 17:39