2024.09.28 Mkutano wa Papa na maaskofu,makleri,watawa,mashemasi,wasemiari na wahudumu wa Kichungaji katika Kanisa la Moyo Mtakatifu la Koekelberg 2024.09.28 Mkutano wa Papa na maaskofu,makleri,watawa,mashemasi,wasemiari na wahudumu wa Kichungaji katika Kanisa la Moyo Mtakatifu la Koekelberg  (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Tahariri

Madhumuni ya Sinodi na mageuzi ya "mtindo"

Maneno ya Papa kwa Kanisa la Ubelgiji na mkutano wa Sinodi ijayo

Andrea Tornielli

Kipaumbele cha Sinodi inayokaribia kuanza ni kipi? Ni lengo gani msingi na muhimu zaidi ya mageuzi katika maana ya sinodi ya Kanisa? Kutoka Buxelles, katika Basilika ya Moyo Mtakatifu ya Koekelberg, mahali ambayo amekutana na Maaskofu, Makleri, Watawa wa kike na kiume na wahudumu wa Kichungaji, Baba Mtakatifu Francisko alichora jibu kwa kuzindua  swali tena. “Mchakato wa sinodi- alisema kwa kuchochewa na kusikiliza ushuhuda - lazima uwe ni kurudi katika Injili; lazima usiwe kati ya vipeumbele vya baadhi ya mageuzi “ya mtindo” bali ni kujiuliza; jinsi gani tunaweza kufanya kufikia Injili katika jamii ambayo haisikilizi tena au imekwenda mbali na imani? Tujiulize wote.”

Si “mtindo “wa mageuzi, kwa hiyo. Si ajenda ambazo - kwa upande mmoja - zinatetea mabadiliko ya kiutendaji na kuishia kuwapa udini wanaume na wanawake walei, wala zile ambazo - kwa upande mwingine - zinalenga kurejesha wakati uliokuwa kwenye wimbi la ukleri  mamboleo: yote mawili ni mitazamo inayoisha ili kufanya irudi nyuma na kulazimisha swali la msingi ambalo Papa Fransisko aliuliza tena, lile la kutangaza Injili katika jamii zisizo za kidini. Yote ni mitazamo inayoishia kusahau lengo pekee la kweli la kila mageuzi katika Kanisa: wema wa roho, utunzaji wa watakatifu, watu waamini wa Mungu.


Kwa kulirejesha swali la Papa katikati, ambalo lilikuwa sababu ya Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican na kwa kurudisha wema na uangalizi wa watu wa Mungu katikati, tunaelewa jinsi gani sinodi ni njia ya kuishi ushirika katika Kanisa. Sio kazi ya ziada ya ukiritimba kwa mapadre na walei ambao wanaikubali kwa kusita na kwa maneno, na matendo ambayo yamebaki kiukweli yamefungwa kwa mitindo ya karne iliyopita. Sio sehemu ya kupita ambayo kwayo tunaweza kuhalalisha kila mpango wa kidunia. Badala yake, ni usemi kamili wa ushirika hai. Kuanzia na kufahamu tu kwamba sisi sote tunapendwa na Mungu, kwa kuishi Injili kwa furaha tu, ndipo tunaweza kuishuhudia kwa ndugu zetu, tukifahamu ukweli kwamba - bila kujali jukumu letu katika Kanisa - tunaitwa na Mwingine; naye Ndiye anayeliongoza Kanisa lake.

Papa Francisko alikutan na maaskofu wa Ubelgiji 28 Septemba 2024
Papa Francisko alikutan na maaskofu wa Ubelgiji 28 Septemba 2024
TAHARIRI YA DK TORNIELLI HUKO UBELGIJI
28 September 2024, 12:13