Jakarta,Papa atembelea Handanki la Urafiki:kutembea pamoja katika nuru kamili
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akitembelea Handaki la Urafiki (Tunnel of Friendship) linalotengenisa Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa na Msikiti Mkuu huko Jacarta nchini Indonesia tarehe 5 Septemba 2024 alitoa hotuba fupi ambapo aliwashukuru wote kwa sababu ya "Harandaki ya Urafiki inayotaka kuwa mahali pa mazungumzo na kukutana. Ikiwa tunafikiria juu ya handaki, tunafikiria kwa urahisi njia ya giza ambayo, hasa ikiwa tuko peke yetu, inaweza kututisha. Hapa, hata hivyo ni tofauti, kwa sababu kila kitu kinaangazwa," amesema Papa na kuongeza kuwa: “Ningependa kuwaambia, hata hivyo, kwamba ninyi ndiyo nuru inayoangazia, pamoja na urafiki wenu, maelewano ambayo mnakuza, msaada wenu wa pande zote, na kwa kutembea kwenu pamoja kunawaongoza, mwisho wa barabara, kuelekea mwanga kamili.”
Papa Francisko akiendelea amesisisitiza kwamba, “Sisi waamini, ambao ni wa mtamaduni tofauti za kidini, tuna jukumu la kutekeleza: kusaidia kila mtu kupitia handaki na wakati macho yetu yakielekezwa kwenye nuru. Hivyo, mwishoni mwa safari, tunaweza kutambua, katika wale waliotembea pamoja nasi, kaka, dada, ambao tunaweza kushiriki maisha na kusaidiana. Kwa ishara nyingi za tishio, kwa nyakati za giza, tunalinganisha ishara ya udugu ambayo, kwa kuwakaribisha wengine na kuheshimu utambulisho wao, inawahimiza kuchukua njia ya pamoja, iliyofanywa katika urafiki, na ambayo inaongoza kwenye nuru.”
Papa ametoa shukurani “kwa wale wote wanaofanya kazi wakiwa na hakika kwamba tunaweza kuishi kwa upatanisho na amani, tukifahamu hitaji la ulimwengu wa kidugu zaidi. “Ni matumaini ya Baba Mtakatifu “kuwa jumuiya zetu zinaweza kufunguliwa zaidi kwa mazungumzo ya kidini na kuwa ishara ya kuishi pamoja kwa amani ambayo ni sifa ya Indonesia.” Na hatimaye Papa Francisko ameinua sala yake kwa Mungu, Muumba wa wote, ili awabariki wote ambao watakatisha hadhini hiyo katika roho ya urafiki,maelewano na udugu.