2024.09.26 Ziara ya Kitume ya Papa Frncisko huko Luxembourg - Kukutana na Mamlaka 2024.09.26 Ziara ya Kitume ya Papa Frncisko huko Luxembourg - Kukutana na Mamlaka  (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Tahariri

Ulaya iliyosahau kumbukumbu na"mauaji yasiyo na maana"

Ni vema kusoma upya hotuba ya Papa Francisko kwa Mamlaka ya Luxembourg.

ANDREA TORNIELLI

Amani, mazungumzo, kazi ya kidiplomasia, maelewano ya heshima... Papa Francisko kutoka Luxembourg, nchi ndogo iliyoko kwenye makutano ya matukio mengi ya kihistoria ya Ulaya, amezindua wito wa amani kwa Ulaya, akiiomba isirudie makosa ya zamani. Ametoa mwaliko Ulaya isiwe msahaulifu. Na usemi wa "mauaji yasiyo na maana" unashangaza katika maneno ya Mrithi wa Petro, ambao unakumbusha ule uliotumiwa na Benedikto XV kufafanua mauaji ya Vita vya Kwanza vya Dunia. Akizungumza na mamlaka ya Luxembourg, Papa alibainisha "kuibuka tena, hata katika bara la Ulaya, migawanyiko na uadui ambao, badala ya kutatuliwa kwa misingi ya nia njema ya pande zote, mazungumzo na kazi ya kidiplomasia, husababisha uhasama wa wazi, na matokeo yao ya uharibifu na kifo."

Je, hatuwezi kufikiria Ukraine ikishambuliwa na Urusi, vita ambavyo tayari vimegharimu wahanga milioni kati ya waliokufa na waliojeruhiwa, na ambayo imeharibu nchi hiyo. Vita vilipigwa kati ya Wakristo wanaoshiriki imani moja, ubatizo uleule na liturujia moja. Kisha  Papa Francisko aliona kwa uchungu kwamba moyo wa mwanadamu unaonekana kutokuwa na uwezo wa "kutunza kumbukumbu." Ndiyo, ni Ulaya iliyosahau, ambayo inahatarisha kurudi kwenye njia ya vita.  Ili kuepusha "mauaji mapya yasiyo na maana", aliongezea, tunahitaji "maadili ya juu na ya kina ya kiroho, ambayo yanazuia wazimu wa akili na kurudi bila uwajibikaji kufanya makosa yale yale ya nyakati zilizopita, kuchochewa zaidi na nguvu kubwa ya kiufundi ambayo mwanadamu wa sasa anachukua fursa hiyo."


Lakini Askofu wa Roma pia alizungumzia wajibu mahususi wa watawala, wa wale walio na mamlaka, akifafanua "haja ya dharura" ya kufanya "kwa uthabiti na uvumilivu katika mazungumzo ya uaminifu kwa nia ya kusuluhisha mizozo". Papa aliomba nafsi ambazo ziko tayari "kutambua maelewano ya heshima, ambayo hayahatarishi chochote na ambayo badala yake yanaweza kujenga usalama na amani kwa wote". Amani, mazungumzo, kazi ya kidiplomasia, maelewano ya heshima: maneno ambayo yanaonekana kutoweka kwenye msamiati wa viongozi, wakiwemo wa Ulaya, katika wakati ambao tunazungumza juu ya silaha tu na mabilioni mangapi ya kuwekeza kwenye vyombo vya kifo.

Ingawa kuna serikali zinazotishia kutumia silaha za nyuklia, wakati idadi ya raia waliouawa na mabomu ya majaribio na drones inaongezeka, wakati nchi zinawekeza kiasi kikubwa katika silaha, kwa kuchukua rasilimali kutoka katika vita dhidi ya njaa, huduma za afya, elimu, ulinzi wa mazingira, ni watu ambao wanapaswa kutoa sauti zao. Maneno yaliyotamkwa na Paulo VI mnamo tarehe 29 Januari 1966 kuhusu usuluhishi za Umoja wa Mataifa juu ya vita huko Vietnam yanabaki kuwa muhimu: "Ni jukumu zito na zito sana kukataa mazungumzo, njia pekee ya kumaliza mzozo bila kuacha silaha, kwa silaha zinazozidi kutisha, uamuzi. Watu wanatazama! Na  Mungu atatuhukumu!”

Siku ya Papa akiwa Luxembourg 26 Septemba 2024
Tahariri ya Dk Tornielli kuhusu Hotuba ya Papa kwa Luxembourg
26 September 2024, 18:02