Tafuta

Papa Francisko amesema, amesikitishwa sana na taarifa za mashambulizi makali ya mabomu huko nchini Lebanon na hivyo kusababisha athari kubwa kwa watu na mali zao. Papa Francisko amesema, amesikitishwa sana na taarifa za mashambulizi makali ya mabomu huko nchini Lebanon na hivyo kusababisha athari kubwa kwa watu na mali zao.   (AFP or licensors)

Wito Kwa Jumuiya ya Kimataifa Kurejesha Amani Nchini Lebanon

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, Jumuiya ya Kimataifa itafanya kila linalowezekana kukomesha mashambulizi haya yanayotishia usalama na maisha ya watu. Papa ametumia fursa hii kuonesha uwepo wake wa karibu kwa wananchi wa Lebanoni wanaoendelea kuteseka kutokana na mashambulizi haya. Imekuwa pia ni fursa ya kusali na kuwaombea watu wanaoteseka kwa vita sehemu mbalimbali za dunia hasa: Ukraine, Palestina, Israeli na Sudan na Mynmar.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 25 Septemba 2024 amesema, amesikitishwa sana na taarifa za mashambulizi makali ya mabomu huko nchini Lebanon na hivyo kusababisha athari kubwa kwa watu na mali zao. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, Jumuiya ya Kimataifa itafanya kila linalowezekana kukomesha mashambulizi haya yanayotishia usalama na maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

Mashambulizi ya mabomu na makombora yamesababisha maafa makubwa
Mashambulizi ya mabomu na makombora yamesababisha maafa makubwa

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuonesha uwepo wake wa karibu kwa wananchi wa Lebanoni wanaoendelea kuteseka kutokana na mashambulizi haya. Imekuwa pia ni fursa ya kusali na kuwaombea watu wanaoteseka kwa vita sehemu mbalimbali za dunia, hasa: Ukraine, Palestina, Israeli, Myanmar na Sudan. Baba Mtakatifu Francisko katika maeneo yote ya vita, anapenda kuwaombea amani ya kudumu.

Papa Lebanon

 

25 September 2024, 14:49