Papa Francisko:tuombee watu wa Valencia na watu wengine wa Hispania wanaoteseka
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 3 Novemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha watu wanateseka kutoka na dhoruba kali iliypiga huko Valencia nchini Hispania huku akihamaisha watu kujitoa kwa moyo katika kuhamasisha msaada wa hali na mali. Papa amesema “Na tunaendelea kuombea Valencia, na watu wengine wa Uhispania, ambao wanateseka sana katika siku hizi. Papa ameomba kujiuliza “ Je nifanye nini kwa watu wa Valencia? Tafadhali, ninaweza kutoa kitu? Fikirieni juu ya swali hili ...”Papa amehitimisha kwa kuwatakia “wote Dominika njema. Na tafadhali msisahau kuniombea. Kuwa na chakula cha mchana mwemma na kwaheri ya kukuona.
Maafa ni makubwa na waathirika ni wengi
Zaidi ya waru 210 wamekufa, lakini bado kuna wengi waliopotea. Matokeo ya janga lililoikumba Valencia ulitolewa na tarehe 2 Novemba 2024 na Waziri Mkuu Pedro Sanchez ambapo bado yanabaki kuwa ya muda. Waziri Sanchez, katika hotuba yake, kisha alitangaza kuwasili kwa askari na mawakala wengine 10 elfu katika eneo lililoharibiwa na dhoruba Dana. Kuna wanajeshi 5elfu, na ndio idadi kubwa zaidi ya vikosi vya jeshi kuwahi kufanywa wakati wa amani, Sanchez alibainisha zaidi. Kufikia sasa, watu 4,800 wameokolewa na watu 30,000 wamesaidiwa.
Mabishano dhidi ya rais wa mkoa
Wakati huo huo, mzozo uliendelea juu ya rais wa eneo hilo Carlos Mazón ambaye inadaiwa hakuwatahadharisha idadi ya watu, akikataa dharura hiyo ili, kulingana na vyanzo vya habari, asilazimike kushughulikia hitaji la msaada wa moja kwa moja. Kwa chaguo la kudumisha kiwango cha dharura cha 2 na kutoiinua hadi kiwango cha 3, ile ya maafa, licha ya idadi kubwa ya vifo, ilimaanisha kwamba Mazón hakuchukulia moja kwa moja amri ya shughuli, na hivyo kutekeleza jukumu lolote la kisheria linalowezekana.
Makadirio ya Chama cha Wafanyabiashara
Chama cha Wafanyabiashara cha Valencia kinakadiria kuwa karibu biashara 4,500 zimepata uharibifu, ambapo karibu 1,800 zinaweza kuharibiwa. Manispaa zilizoathiriwa zingekuwa mwenyeji wa zaidi ya 30% ya wakazi wote wa jimbo la Valencia. Na wakati huo huo, maelfu ya watu wanaendelea kufika katika maeneo yaliyoharibiwa kupeleka msaada wao, ni vijana kwa wazee, wajitolea ambao wamefika kutoka nchi nzima kwa njia zao za kufika sehemu zilizotengwa zaidi ambazo bado hazijafikiwa kwa msaada.
Uokoaji wa mwanamke
Hata hivyo, matumaini bado ni makubwa kwamba bado wataweza kuwapata watu wakiwa hai, uokoaji wa tarehe 2 Novemba wa mwanamke ambaye alinaswa kwa siku tatu kwenye gari lililotelekezwa mwishoni mwa njia ya chini katika moja ya vituo vilivyoathiriwa zaidi na mafuriko iliwapa matumaini zaidi.