Papa Francisko:vita vipigwe marufuku,tuombee nchi zenye vita!
Na Angella Rwezaula - vatican
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 3 Novemba 2024, akiwageukia waamini na mahujaji wengi sana waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu Franciko alianza na salamu kwamba: “Ninawasalimu ninyi nyote, Warumi na mahujaji kutoka Italia na nchi zingine!
Amewasalimu Masista Wamisionari Wakarmeli wa Roho Mtakatifu, wanaoadhimisha miaka ishirini na mitano ya udugu wao wa kilimwengu; Amewasalimu waamini wa Venezia, Pontassieve, Barberino ya Mugello, Empoli na Palermo, na wa Mtakatifu Maria wa Fornaci huko Roma; pamoja na vijana wa Catanzaro wakiwa na waelimishaji wa parokia zao. Amewasalimu wachangiaji damu wa Coccaglio (Brescia).
Papa aidha amewasalimu kikundi cha Dharura ya Kusini mwa Roma kilichojitolea kukumbuka Kifungu cha 11 cha Katiba ya Italia, kinachosema: “Italia inakataa vita kama chombo cha kosa dhidi ya uhuru wa watu wengine na kama njia ya kusuluhisha mizozo ya kimataifa". Papa ameomba “Kumbuka makala hii. Endeleeni mbele!”Na kanuni hii inaweza kutekelezwe duniani kote: vita vipigwe marufuku na masuala yashughulikiwe kupitia sheria na mazungumzo. Silaha zinyamazishwe na kutoa nafasi kwa mazungumzo.” Amesema Papa Papa akiendelea Papa amesema “Tunawaombea wanaoteswa Ukraine, Palestina, Israel, Myanmar, Sudan Kusini.