Wito wa Papa tusisahau nchi zinazopigana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya katekesi yake Jumatato tarehe 13 Novemba 2024, Papa Francisko kwa akisalimia wanaozungumza lugha ya kiitalino alisema “Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, ninawasalimu Polisi wa Jimbo la Campobasso na Isernia, 50&PIÙ Chamacha Lombardia, Taasisi ya damu Azizi ya Milano, Bendi ya Giuseppe Verdi ya Vallecorsa. Ilicheza vizuri, basi tutawasikiliza wakati mwingine ...”
Hatimaye, mawazo yake yaliwaendea vijana, wagonjwa, wazee, na wanandoa wapya: “Ninawahimiza kila mtu kupata nguvu na ujasiri katika Mungu kila siku ili kuishi wito wao wa kibinadamu na wa Kikristo kikamilifu.”
Wito kwa amani
Papa Francisko kwa maskitiko amesema “Na tusisahau nchi zilizopigana. Ndugu na dada, Ukraine inayoteswa inateseka! Tusiisahau Ukraine; tusisahau Palestina, Israel, Myanmar na mataifa mengi kwenye vita. Tusisahau kundi hilo la Wapalestina waliopigwa risasi na bunduki, wasio na hatia... Tuombe amani. Tunahitaji sana, tunahitaji sana amani!”
Wapoland
Papa alisema: “Ninawasalimu kwa moyo mkunjufu mahujaji wa Poland. Katika masuala yenu ya kibinafsi, ya kifamilia na kijamii, ombeni msaada wa Mama wa Mungu, Malkia wa Poland, ambaye amelilinda taifa lenu katika nyakati ngumu sana. Mmeadhimisha kumbukumbu ya kurudi tena kwa uhuru, ambayo watu wa Kipoland walipigana hata na rozari mikononi mwao. Heshumuno moya wa mama wa Maria kwa shukrani. Nawabariki wote.”
Kwa lugha ya kijerumani
“Ninatoa salamu kwa mahujaji wote, hasa kwa kikundi cha Caritas kutoka Jimbo kuu la Alba Iulia nchini Romania. Tujikabidhi kwa Bikira Maria, Binti wa Baba, Mama wa Mwana, Bibi-arusi wa Roho Mtakatifu atusaidie daima kubaki katika upendo wa Mungu wa Utatu anayetufanya kuwa ndugu na kutusukuma kuishi hivyo. Baba Mtakatifu: “Nawasalimu waamini wanaozungumza Kiarabu. Hebu tufanye upya "ndiyo" yetu kwa Bwana na mapenzi yake pamoja, tukimtumaini Yeye, kama Maria. Hivyo atatupatia maisha mapya na bora. Bwana awabariki nyote na kuwalinda daima na mabaya yote!