Tafuta

Ukuta uliochorwa Picha ya Papa katika matarisho ya Ujio wake huko Ajaccio-Corsica Ukuta uliochorwa Picha ya Papa katika matarisho ya Ujio wake huko Ajaccio-Corsica  (AFP or licensors)

Papa kwenye hija Corsica,kati ya Udini Maarufu na changamoto za Mediteranea!

Tarehe 15 Desemba 2024 Papa anatarajia kufanya Ziara ya 47 ya Kitume kwenda Corsica.Ni ziara ya haraka huko Ajaccio chini ya masaa 12 ili kufunga Kongamano la Udini Maarufu wa Watu wa Mungu,kukutana na makleri na Misa mbele ya waamini elfu 7.Dk.Bruni:"Maneno ya ibada yanasikika sana nchini Ufaransa,ni hotuba zenye mwangwi wa migogoro ya Mediterania."Papa atatoa heshima kwa Maria na atakuwa na mazungumzo ya faragha kwenye Uwanja wa ndege na Macron.

Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.

Ziara ya kitume ya Papa Francisko itaaanza Dominika tarehe 15 Desemba  2024 hadi huko Corsica, nchi ya asili ya Napoleon, "Île de beauté", kama inavyoitwa kuwa "kisiwa cha uzuri" na mandhari yake iliyopangwa na misitu, fukwe na milima, lakini  hatari ya migogoro ya mazingira inayochochewa na binadamu. Hata hivyo kwa upande mmoja, ni ucha Mungu au udini maarufu, imani ya rahisi, iliyooneshwa katika safari, matendo ya ibada katika mahali patakatifu, maandamano na nyimbo za kiutamaduni. Kwa upande mwingine, Bahari ya Mediterania na changamoto zake, matukio ya vita, janga la ajabu la uhamiaji ambao umefanya Mare Nostrum, yaani Bahari yetu kuwa "makaburi ya wazi," ambayo Kongamano atakalofunga Papa litajikita na mada kama hizo.

Ni ziara ya 47 ya Kitume huko Corsica

Hii ni ziara ya 47 ya Kitume ambapo Jorge Mario Bergoglio anafikisha idadi ya nchi 67 zilizotembelewa, na hii ambayo itkuwa kwa siku moja tu ya masaa ikilinganishwa na hija ndefu ya mnamo Septemba hadi Kusini-Mashariki mwa Asia na Oceania. Chini ya masaa kumi na mbili ambayo pia yatamuona Papa  Francisko ana kwa ana kwa takriban dakika arobaini akiwa na rais wa Ufaransa, Bwana Emmanuel Macron kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege kurudi Roma jioni.

"Francescu", Papa wa kwanza huko Ajaccio

Pia  hii ni ziara ya kwanza ya Papa katika mji mkuu wa Ajaccio, lakini si ya Papa wa baadaye ikizingatia ile ya Angelo Roncalli, ambaye baadaye alikuja kuwa Papa JYohane  XXIII, wakati kakiwa ama Balozi wa  Vatican jijini Paris alipotembelea kisiwa hicho mnamo mwaka 1952. Huu ni ukweli wa kihistoria uliokumbukwa na Msemaji wa  Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni, katika mkutano wa kawaida na waandishi wa habari watakaomfuata na Papa Francisko  katika ziara  yake ya kimataifa. Kwa mujibu wa Dk Bruni alisema kuwa: "Papa anasonga mbele kukutana na Wakristo wa kisiwa hicho na kwa mkutano wa watu udini maarufu wa Watu."

Papa atahutubia hotuba tatu

Kwa kurejea Mada ya Kongamano la “de La religiosité populaire en Méditerranée,” ambayo ni hafla ya siku mbili iliyoandaliwa na Askofu wa Ajaccio, Kardinali François-Xavier Bustillo, ambayo itashuhudia uwepo wa washiriki zaidi ya 400, wakiwemo maaskofu wa Hispania, Ufaransa, Italia, wasomi, na wawakilishi wa maeneo mengine yanayoelekea Mediterania. Papa Francescu atawahutubia - kama inavyoweza kusomwa katika nembo ya bluu ya ziara hiyo, katika lugha ya Kikorsika - katika hotuba yake ya kwanza kati ya tatu (zote kwa Kiitaliano) ambazo zitafunga Kongamano hilo. Heshima kwa "Madonnuccia yaani “Mama" ambaye alikomboa kisiwa kutokana na janga la tauni, itakuwa tafakari juu ya mada ya udini maarufu ambayo inasikika sana Ufaransa yo," alisema Bruni.

Asilimia 80 ya wakati ni wakatoliki na ibada ya Maria inasikika sana

Hii hasa katika Corsica, ambapo 80% ya wakazi ni Wakatoliki na ambapo kuna udugu na ibada ya "Madonnuccia",Mama  Bikira Maria ambaye kunako mwaka 1656 alikilinda kisiwa hicho, kisha chini ya utawala wa Genoese, kutokana na tauni, na kubadilisha mwendo wa upepo ambao ulizuia meli zilizobeba wagonjwa kutia nanga katika Ajaccio. Muujiza, huo kulingana na maelezo  ni kwamba  ulizuia kuenea kwa janga kwenye kisiwa hicho.

 

Papa atasali mbele ya picha na kuwasha mshumaa

Tangu wakati huo "Madonnuccia" yaani Bikira maria  imekuwa ikiheshimiwa kama mtakatifu Msimamizi na mlinzi na sherehe kubwa imetolewa kwake katikati ya  Mwezi Machi kila mwaka. Picha ya Mamama, iliyopo kwenye nembo, itaambatana na ziara ya upapa. Papa atatoa heshima kwa sanamu ya Marian "kwa muda wa kutafakari" na kuwasha mshumaa, katikati ya njia kati ya umati wa watu ambao utampeleka kwenye maeneo mbalimbali ya matukio.

13 December 2024, 17:03