Papa ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kard.Amato
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 1 Januari 2025 ametuma telegramu ya rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Angelo Amato kilichotokea tarehe 31 Desemba 2024 akiwa na umri wa miaka 86. Katika salamu zake Papa alimtumia Padre Stefano Martoglio(SDB) Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Francis wa Salas(Salesian),Roma akibainisha “kupokea taarifa za kuondokewa na mpendwa huyo, na hivyo kuelezea ukaribu wake kwake na ndugu wengine wa shirika hilo la kidini, ikiwa ni pamoja na wanafamilia wanaoomboleza kwa kifo chake.”
Ushuhuda wa kujenga
Baba Mtakatifu Francisko “anamshukuru Mungu kwa ushuhuda wa kujenga wa Mtoto wa kiroho wa Mtakatifu Yohane Bosco ambaye kwa miaka mingi alijituma na wema na ukaribu wa binadamu kwa ajili ya Injili na Kanisa.” Papa “amefikira juu ya nafasi yake ya kikuhani na maandalizi ya kitaalimungu aliyowahudumia watakatifu hasa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu.”
Kuombea roho ya mtumishi wa Mungu
Kwa njia hiyo Papa Francisko “anamwahakikishia sala zake kwa roho ya Mtumishi huyo mwema na anayekesha, mwaminifu katika kauli mbiu yake “Sufficit gratia mea,” yaani “Neema yako yatosha,” hata katika “siku za hivi karibuni zilizokuwa na mateso, alijiachia katika wema wa Baba wa Mbinguni.” Papa anaamini “kwamba kwa kusindikizwa na Maria Msaada wa Wakristo, na watakatifu, na Wenyeheri aliowaongoza katika utukufu wa Altareni, Yeye atakaribishwa katika meza ya milele mbinguni.” Kwa kuhitimisha Papa amewatumia “Baraka wote wanaoshiriki uchungu wa kuondoka kwake.”