Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Frolicsome Finale - Prestissimo con fuoco
Ratiba Podcast
2025.04.06 Papa akisalimiana na wale waliokuwa wasome shukrani zake kwa lugha mbali mbali. 2025.04.06 Papa akisalimiana na wale waliokuwa wasome shukrani zake kwa lugha mbali mbali.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:"Asante sana,Jubilei iwe na matunda tele"

Baada ya kuwapa baraka akiwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Domika 6 Aprili 2025,Papa aliacha uwanja na kukabidhi wamsomee shukrani zake za upendo wale wote walioshiriki katika maadhimisho haya na kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa sala iliyoinuliwa kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya afya yake,akitumaini kwamba,hija ya Jubilei hiyo itakuwa na matunda tele.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Na kabla ya Baraka ya mwisho, yaani mwishoni mwa Misa, Baba Mtakatifu  Dominika tarehe 6 Aprili 2025 alifika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,mbele ya madhabahu na kutoa maneno machache akisema: “Dominika njema kwa wote. Asante sana.” Baadaye Baba Mtakatifu Francisko aliacha Uwanja huo na baadaye kusomwa kwa lugha mbali mbali, maneno ya shukrani ya Papa Francisko.

Maneno hayo yalikuwa yanabainisha kuwa Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia kwa upendo wale wote walioshiriki katika maadhimisho haya na kuwashukuru kwa dhati kabisa sala iliyoinuliwa kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya afya yake, akitumaini kwamba, hija ya Jubilei hiyo itakuwa na matunda tele, amewapatia baraka za kitume, akiwapa wapendwa wao, wagonjwa na wanaoteseka, pamoja na waamini wote waliokusanyika leo. Vikundi vifuatavyo viliripoti uwepo wao katika hafla hiyo: kutoka Italia, Jimbo la  Vittorio Veneto na Jimbo la  Termoli-Larino. Pia kuna vikundi vya wamini kutoka Albania na Kroatia.

Papa ashukuru
06 Aprili 2025, 16:14
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031