Lombardi:Papa Ratzinger hajawahi kuficha mabaya katika Kanisa

Rais wa Mfuko wa Vatican"Joseph Ratzinger-Benedikto XVI",naambaye alikuwa msemaji wa zamani wa Papa Mstaafu:"Kama mhudumu ninaweza kushuhudia kwamba kwake yeye huduma ya ukweli daima likuwa na nafasi ya kwanza hata kwa kile kilichokuwa ni kichungu."

Na Angella Rwezaula – Vatican

Katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Vatican na Padre Federico Lombardi ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Vatican wa “Joseph Ratzinger – Benedikto XVI”, na aliyekuwa ni msemaji wa zamani wa Papa mstaafu akitoa maoni juu ya Barua ya Papa Mstaafu  iliyochapishwa kuhusu Ripoti ya Munich juu ya nyanyaso amethibitisha kushangazwa na uwazi wake na kina chake. Kama asemavyo katika maandishi ya barua, aliishi katika kipindi cha uchungu ambapo alifanya uchunguzi wa dhamiri, yeye mwenyewe: juu ya maisha yake, juu ya tabia yake na  juu ya hali ya Kanisa leo hii. Alitafakari juu ya hilo katika barua ambayo ni tokeo la wakati mzito, wenye uchungu wa uchunguzi wa kweli mbele za Mungu. Ni mtu mzee, ambaye anajua kwamba anaelekea kukutana na Bwana na kwa hiyo kuelekea hukumu ya Mungu, na hii inazungumza juu ya uaminifu mkubwa wa  kina cha maandishi na jinsi anavyoishi jibu hili analitoa, baada ya kipindi ambacho kwa hakika kilikuwa cha kutafakari na mateso kwake, lakini pia mjadala mkubwa katika Kanisa, wa kuchanganyikiwa. Yeye anatoa ushuhuda wake, msaada wa kuona hali na matarajio kiukweli, kwa uwazi na kwa uaminifu na utulivu.

Akijibu juu ya swali kuhusu kurudia maneno ya  “mea maxima culpa” inayorudiwa kila wakati katika Misa na nini maana ya kuomba msamaha uliomo katika barua , Pad Padre ombardi  amesema kuwa Papa mstaafu  anajiweka katika hali ambayo anaishi kila siku, kuadhimisha Ekaristi. Mwanzoni mwa Misa kuna ombi hilo la msamaha kabla ya kukutana na Bwana, na yeye huliishi kwa undani sana. Na hiyo inahusisha tafakari yake yote juu ya hali yake binafsi na hali ya Kanisa ambayo anahisi kuhusika nayo. Kwa hivyo anatoa maneno haya ambayo tumerudia mara nyingi , nimekosa mimi, nimekosa mimi , nimekosa sana  ambayo ni  nguvu kubwa. Anajaribu kuona kwa uwazi kabisa ni nini hatia hiyo kubwa ambayo yeye pia anahisi kuhusika, katika mshikamano na Kanisa zima. Na anabainisha kwamba katika wakati huu na wakati wake wa kutafakari, ni hatia kubwa ambayo historia  nzima ya unyanyasaji wa kijinsia inahusisha. Anafanya tafakari hii ya toba mbele ya wahathirika wa unyanyasaji Inaibua mikutano aliyokuwa nayo na waathirika na maarifa ya kina zaidi ya uzito wa mateso ya waathirikaa na matokeo ambayo yanatokana na nyanyaso hizi. Anajidhihirisha, kwa uaminifu mkubwa na kwa njia ya wazi sana, aibu, maumivu, ombi la dhati la msamaha. Haya ni maneno ambayo katika miaka ya hivi karibuni pia tumeyasikia kwenye midomo ya Papa Francisko na ni yale ambayo yanarejea kwa undani kutoka kwake pia, ambaye anapitia tena historia yake  juu ya mada ya nyanyaso kutokana uzoefu wake wa kwanza katika jimbo la Munich hadi uwajibikaji aliokuwa nao  Roma, kama Papa mwenyewe.

Tafakari yake hii haipaswi kuzingatiwa kama ya kufikirika na ya jumla, lakini ni halisi: anarejeea ukosefu wa umakini kwa waathirika, kwa usingizi wa wanafunzi mbele ya mateso ya Yesu, ambayo kwa asili pia ni pamoja na mateso ya waathirika; kutojitoa kimaamuzi vya kutosha ili kupambana na balaa  hii na uhalifu huu… Kwa hiyo anarejeea kwa usahihi kabisa ukweli huu, haendelezi mazungumzo ya kidhahania na ya jumla. Kwa maana hiyo, mwishowe ombi lake la msamaha kutokana na  hatia mbele ya Mungu  la kumwombea, likielekezwa kwa Mungu, vile vile  kwa kaka na dada zake, kwa hiyo kwa waathirika kama hao na kwa jumuiya yote ya Kanisa inayojisikia kuhusika katika jambo hili kuu. Swali pana sana ambalo anahisi kuhusika nalo na kuona ukweli wote wa uzito wa historia hii kuwa ni kitu ambacho mtu anapaswa kuomba msamaha, kujitakasa na kujitolea kwa nguvu zake zote kubadili mtazamo wake na kuwa mwaminifu zaidi kwa hitaji la Injili.

Na kuhusiana na shutuma kuhusu ushiriki wa  mkutano 1980 wakati iliamuliwa kumkaribisha padre mnyanyasaji katika jimbo la Munich, Padre Lombardi anasema pia kuna kumbukumbu katika barua ya Papa Mstaafu na kisha kuna maelezo ya kina zaidi katika nyongeza ambayo imechapishwa, iliyotiwa saini na washauri, na wataalamu wa sheria ambao wamemsaidia Papa katika kujibu pingamizi, zote mbili katika jibu la kwanza walilopewa, sasa liko kwenye ufupisho wa mwisho juu ya suala hili. Kulikuwa na jibu la kwanza, refu, katikaa  kurasa 82 zilizotolewa kwa wale waliokuwa wakitayarisha Ripoti, kosa moja: ilisemekana kwamba Papa hakuwa amehudhuria mkutano. Siku chache tu baada ya kuchapishwa kwa Ripoti hiyo, Papa Mstaafu  mwenyewe , siku zote,  kwa kawaida alikuwa na taarifa ambayo alisema: “Hapana, hiyo sio kweli: nilihudhuria mkutano huu, na nitawaomba wannifafanulie jinsi ilivyotokea kosa hili ambalo limeamsha aina fulani tuseme la kuchanganyikiwa, bila shaka, na miangwi  fulani. Na katika kiambatisho, walioandaa jibu hili wanaeleza jinsi hili lilivyotokea katika mchakato wa kuandaa jibu hili refu. Walakini, wanaelezea kwamba hii haiathiri ukweli kwamba askofu mkuu  wa wakati huo Ratzinger , hakujua ukweli wa shtaka la unyanyasaji dhidi ya kasisi huyo na kwamba kwa hivyo kosa ni matokeo ya uangalizi katika uhariri, lakini si jambo ambalo lilikuwa limeandikwa kwa kujua kukataa kuwepo (ambalo, zaidi ya hayo, lilitokana na itifaki ya mkutano na hali nyinginezo) na kwamba kwa hiyo hapakuwa na sababu ya kukataa.

Padre Lombardi amesema: “Hapa, sasa, nisingeingia kwa undani sana. Jambo ni hili: Papa Mstaafu aliteseka kutokana na shutuma hii kwamba alifanywa kuwa mwongo, kwa kujua uwongo juu ya hali halisi. Si hivyo tu, bali pia katika ripoti kwa ujumla, shutuma hizo zinakuwa kwa kujua ni siri ya wanyanyasaji, na hivyo kukosa umakini na dharau kwa mateso ya waathirika. Baadaye Papa mstaafu alijibu: “Hapana, mimi si mwongo. Shtaka hili lilinisababishia mateso makali, lakini ninathibitisha kwamba mimi si mwongo.” Lazima niseme, pia binafsi, kwamba nina hakika kabisa, nadhani ni sawa kwamba anadai ukweli wake”.  Kwa sababu ni tabia ya utu na tabia yake katika maisha yake yote, ambayo ninaweza pia kushuhudia, baada ya kuishi karibu naye kama mshiriki kwa miaka kadhaa: huduma ya ukweli daima imekuwa mahali pa kwanza. Hakujaribu kamwe kuficha kile ambacho kingeweza kuwa chungu kwa Kanisa; hajawahi kujaribu kutoa picha nzuri ya uongo ya ukweli wa Kanisa au ya kile kinachotokea. Kwa hiyo naamini kabisa kuwa ukweli wake hauwezi kutiliwa shaka kwa namna yoyote ile. Na hili yeye mwenyewe anathibitisha, naamini ni sawa kumkaribisha kwa ujasiri na imani.

08 February 2022, 17:59