Kard.Krajewski:shukrani kwa nchi zilizo karibu kuwakabirisha watu nyumbani mwao
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ujumbe wa Papa Kupitia Kardinali Konrad Krajewski wa ukaribu na msaada unaendelea. Kwa maagizo ya Papa aliyemtuma nchini Ukraine, Msimamzi wa sadaka ya kitume anaendelea na ziara yake kwa watu wanaoteseka na leo hii, baada ya kusimama huko Lviv, alifika Rivne, kaskazini-magharibi, ambapo alitembelea baadhi ya jumuiya za Kikatoliki za mji huo kwa kushiriki katika sala ya kiekumene kwa ajili ya amani na kukutana na watu wa wanaojitolea kukidhi mahitaji ya watu.
Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, Kadinali alisisitiza juu ya ukaribu wa Papa Francisko kwa Ukraine, kwamba anataka kusema kkuwa anaipenda Ukraine, anaiombea Ukraine na kuunganisha ulimwengu mzima na Ukraine”. Akikumbuka ziara ya Papa Francisko kwenda kwenye Ubalozi wa Urusi siku ya kwanza ya mzozo, Kardinali Krajewski amesema kuwa Papa alikwenda kuomba huruma, ili watu wasife. Baba Mtakatifu anafuata mantiki ya Injili, hii ina maana kwamba imani inaweza kuhamisha milima. “Silaha yetu ni imani. Ikiwa tunaamini tu, tunaweza kupata huruma na amani yake kwa ajili ya Ukraine kutoka kwa Mungu”.
Kardinali Krajewski baadaye alisisitiza kwamba Papa anasali kila siku kwa ajili ya Ukraine, na kwamba dhamira yake ni kuwajulisha kuwa: “Baba Mtakatifu anafahamu kila kitu kinachotokea Ukraine: anajua jinsi watu wanavyoteseka, jinsi anavyotoroka na jinsi kila mtu anavyoteseka na kukaribishwa Ulaya. Hivyo shukrani kwa nchi jirani kwa sababu wanakaribisha watu wa Ukraine katika nyumba zao. “Mungu ibariki Ukraine”, salamu yake ya mwisho.