Papa,Sudan Kusini:Kauli mbiu:“Ninawaombea ili wote wawe na umoja"
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Jumatato tarehe 23 Machi 2022, imetolewa Kauli mbiu inayoongoza ziara ya Kipapa ya Sudan Kusini kunzia tarehe 5 hadi 7 Julai 2022 isemayo: “Ninaomba ili wote wawe na umoja”, ambayo imetolewa katika kifungu cha sala ya kikuhani ya Injili ya Yohane 17. Nembo ya ziara hiyo ina Njiwa ambapo imezungukwa na ramani ya Sudan Kusini kwa rangi za bendera yake, Msalaba na mikono miwili iliyoshikana na Pembeni mwa bendera ya Sudan Kusini ametua Njiwa ambaye amebeba tawi la mzeituni unaowakilisha shauku ya amani kwa anjili ya Nchi.
Mikono iliyoshikana kuwakilisha upatanisho
Juu ya Bendera ametua Njiwa inayonesha Sudan Kusini katikati ya baendera kuna mikono miwili liyoshikana inawakilisha upatanisho wa makabila ambayo yanaunda Taifa moja.
Msalaba urithi wa historia na ishara ya mateso
Kulia kuna msalaba uliosimama na ambao unawakilisha urithi wa Nchi na historia yake ya Mateso. Karibu na msalaba kuna neno lilioandikwa “Papa Francisko nchini Sudan Kusini na tarehe ya ziara yake ya kitume 5-7 Julai 2022.