Tafuta

Papa Francisko atashikiri Mkutano wa Sala ya Amani " Kilio cha Amani" 25 Oktoba 2022 ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Papa Francisko atashikiri Mkutano wa Sala ya Amani " Kilio cha Amani" 25 Oktoba 2022 ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio 

Papa atashiriki Mkutano kuhusu "Kilio cha Amani"

Msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Bruni,amebainisha juu ya ushiriki wa Papa katika Mkutano wa sala kwa ajili ya kuombea amani ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio tarehhe 25 Oktoa kwa kuongoza na kauli mbiu “Kilio cha amani”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa kujibu mswali ya waandishi wa habari Dk. Matteo  Bruni , Jumanne tarehe 11 Okotba 2022, amesema kuwa Baba Mtakatifu atashiriki Mkutano wa Sala kimataifa  kwa ajili ya kuombea  Amani duniani  na wawakilishi viongozi wakuu   kidini Ulimwenguni, ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambao unaongozwa na kauli mbiu: Kilio cha Amani,” utakofanyika tarehe 25 Oktoba  katika Magofu jijini Roma. Mkutano wa mwaka jana ulianza tarehe 6 hadi 7 Septemba 2021 kwa ushiriki na uwepo wa viongozi wakuu wa kidini kutoka sehemu mbalimbali za duniani, akiwemo Baba Mtakatifu Francisko ambapo uliongozwa na kauli mbiu  “Watu ndugu, Ardhi ya baadaye.”

Mkutano wa kuombea amani ulimwenguni
Mkutano wa kuombea amani ulimwenguni

Amani ya kweli inajengwa katika msingi wa maendeleo endelevu ya binadamu: kiroho na kimwili; kanuni maadili na utu wema; utawala wa sheria na haki msingi za binadamu! Vita, sawa na  mipasuko ya kijamii ni hali halisi ya maisha ya binadamu yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa kujikita katika kanuni maadili, sheria za kimataifa ikiendana na ujenzi wa siasa ya amani duniani ambayo inajikita na majadiliano katika ukweli na uwazi. Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akikazia hayo na kwamba  Jumuiya ya Kimataifa haina budi kuwekeza katika mchakato wa ujenzi wa utamaduni wa amani duniani; upendo na mshikamano wa udugu wa kibinadamu majadiliano pamoja kwa kulinda na  kudumisha haki msingi za binadamu, uhuru pamoja na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya pamoja.

Papa atashiriki Mkutano wa amani tarehe 25 Oktoba
11 October 2022, 13:19