Askofu mpya msaidizi wa Jimbo kuu katoliki la Durban,Afrika Kusini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Alhamisi 9 Machi 2023, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu latoliki la Durban (Afrika Kusini ) Mhs. Elias Kwenzakufani Zondi, wa jimbo kuu hilo ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni makamu Mkuu na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu James huko Lamontville, na kupatiwa makao ya Rutabo.
Wasifu wake: Askofu Mteule Elias Kwenzakufani Zondi alizaliwa mnamo tarehe 24 Desemba 1963. Baada ya majiundo ya Seminari ya Malezi ya Mtakatifu Paulo ya Hammanskraal, aliendelea na masomo ya Falsafa katika seminari Kuu ya Mtakatifu Petro ya Garsfontein na baadaye ile ya kitaalimungu ya Mtakatifu Yohane Vianney huko Pretoria. Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 16 Julai 1994 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Durban.
Nyadhifa nyingine: Askofu Mteule amekuwa Vika paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme huko Wentworth (1994-1995); Paroko wa Mtakatifu James huko Mooi River (1996-2000); Paroko wa KwaKristo Umsindisi na Mama Yetu wa Lourdes (2001-2015); na tangu 2016, Paroko wa Mtakatifu James huko Lamontville; wakati huyo mnamo 2021, amekuwa makamu Askofu