Tafuta

Kardinali ametia saini kwenye tamko lililoandaliwa na washindi wa Tuzo ya Nobel wakati wa Mkutano wa kimatafia kuhusu Udugu wa kibinadamu. Kardinali ametia saini kwenye tamko lililoandaliwa na washindi wa Tuzo ya Nobel wakati wa Mkutano wa kimatafia kuhusu Udugu wa kibinadamu.  (AFP or licensors)

Kard.Parolin:ulimwengu unahitaji matumaini na udugu wa kibinadamu

Mkutano wa Kimataifa wa Udugu wa Kibinadamu ulifunguliwa kwa mkutano wa vikundi 5 vya kazi:Washindi wa Tuzo ya Nobel,mazingira,shule,walio hatarini na vyama.Kardinali Paroliniamesema wamekusanyika kama ishara ya matumaini kwa ulimwengu.Uwepo tayari ni ishara ya matumaini.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumamosi jioni tarehe 10 Juni 2023 imefanyika Mkutano wa kimataifa juu ya Udugu wa Kibinadamu unaoongozwa na mada :“Not alone,” yaani Siyo peke yake”, ulioandaliwa na Mfuko wa Vatican wa Fratelli Tutti, kwa ushirikiano na Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu na  pamoja na Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Katika mkutano huo, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, ametoa hotuba yake akianza na kuwakaribisha na kuwashukuru kwa maneno ya utangulizi wa kazi yao na hasa kwa kukubali mwamko wa pendekezo la Kardinali Mauro Gambetti na Mfuko wa Fratelli tutti kukutana ili kuhamasisha amani na haki kati ya watu katika Mkutano wa Kwanza kuhusu ‘udugu wa kibinadamu’. Kufanya kazi katika roho ya udugu ni uwajibikaji ambao hauwezi kuacha kwa yule anayeitwa kuhuisha utumaduni wa mahusiano ya kimataifa. Wengi wao kwa njia ya chaguzi  na ishara walizotimiza katika maeneo ya migogoro, inajionesha  wazi kwa mifano ya maisha ambayo kwa kukatisha mazungumzo na uhusiano wake ambao udugu  unaunganisha ni zaidi ya nguvu ya uchungu ambao unagawanya.

Kilichotendeka katika Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu

Wengi wao Kardinali Parolin alisema wanaweza kushuhudia kama kusuka kwa uvumilivu mtego wa mazunguzo jinsi ulivyo mgumu na mara nyingi wa masumbuko  sio kidogo lakini adhimu na kuwa kwa ajili ya wema wa jumuiya ya kibindamu, iwe kwa ngazi mahalia na ile ya kimataifa. Utafiti wa ushirikiano katika ya Nchi, ni uthibitisho wa kwanza wa haki juu ya nguvu  jitihada kwa ajili ya maendeleo fungamani ya binadamu  na kwa ajili ya uchumi kwa kipimo cha shauku ya haki kwa watu wote ni kielelezo kikubwa cha kujikita nacho na ambacho kinatusukuma kufanya kazi bila kuchoka ili pasiwepo mwanamke na mwanamme katika Sayari hii kuweza kuhisi kubaguliwa na familia ya binadamu. Kwa hakika kukutana kidugu kunapendekeza kushikamana mikono na kutupeleka ili kuchuka nafasi kwa yule ambaye anafikiri tofauti nasi na baadaye kujifungua katika upamoja milango ya tumaini, ya kushirikishana na mielekeo ambayo ubinadamu unaweza kutuweka pamoja kwa kuwa na vipimo vya utunzaji wa hatua kwa hatua ili kila mmoja aweza kutafufa safari ya pamoja ambaye hakuna anayebaki nyuma.

Hamasa hii  ya mshikamano na maongozo kwa ajili ya ukimya zaidi unaanzia  upande wa mtu, ili kukumbatia ukuu wa kifamilia, ule wa kijamii na wa mataifa hadi kutikia Jumuiya nzima ya kimataifa. Ni safari inayofanywa ili kukabiliana na msukumo wowote wa kiutendaji ambao mara nyingi, kwa bahati mbaya, leo hii huwaweka watu kwa watu binafsi, nyuso kwa idadi, miradi ili kupata faida. Ni njia ambayo huchota kutoka katika kina cha mwanadamu, kiumbe hai cha asili yake ya uhusiano, mwenye uwezo wa kutokuwa na mwisho na kuwafikia wanadamu wenzake, shukrani ambayo yeye hukua mwenyewe. Hekima ya kiutamaduni inatukumbusha hili, kulingana na ambayo yote ni kubwa kuliko jumla ya sehemu zake, amesisitiza Kardinali Parolin. Hata hivyo Kardinali Parolin ameuliza swali ambalo amesema  mara kadhaa limemjia“hata kama mawazo na majaribio ni mazuri, je, inafaa? Je, inafaa kusafiri, kukutana na kuzungumza na kila mmoja katika ulimwengu unaoonekana kufuata mantiki nyingine kuliko zile za udugu na kukutana? Kwa kujibu amesema katika Waraka wa Fratelli tutti wa Papa Francisko kiukweli utafikiri ni jibu la maswahi hayo kwa kuthibitisha kuwa “mazungumzo ya kudumu na ya kijasiri hayafanyi habari kuwa kama migongano na mizozo, lakini kwa busara husaidia ulimwengu kuishi vizuri zaidi kuliko tunavyofahamu (Ft 198). Kwa hivyo Papa anapendekeza kukuza sio tu hali ya kiroho ya udugu, lakini ushirika wa  ulimwengu wenye ufanisi zaidi, wa kusaidia kutatua shida kubwa.” (Fratelli tutti, 165).


Kardinali Parolin amebainisha kwamba katika fursa nyingine aliweza kubainisha jinsi gani ya kujielezea udugu na kufanya urafiki wa kimaadili katika wazo ya kuendelea labda ambalo halitoshi. Na kwa wakati huo huo mahusiano ya kimataifa ambayo hayawezi kutofautiana na lengo la amani ambayo inaeleweka kama ukosefu wa vita na wala usalama, katika maendeleo au katika kulinganisha na matendo ya haki msingi. Wakati matendo ya kidiplomasia yanapaswa kuongeza nguvu katika nafasi ya mashirika ya kimataifa na hii ni kipaumbele cha kweli katika matendo kwa matazamio ya kimataifa ambayo anaamini kwamba ni muhimu, kama hatua ya kwanza, kurejea kwenye maana ambayo Baba Mtakatifu anaitambua katika udugu anapoipendekeza kama msingi madhubuti, ambao ndiyo kiini cha ajenda za kimataifa; na kama ambapo pia alipenda kusema, wito wa ulimwengu wote, ambao unatambulika kwa dhati kuanzia kila mmoja, kuanzaia na mtu binafasi  wakati sisemi tena kwamba nina majirani wa kusaidia, lakini ninahisi kuitwa kuwa jirani na wengine (Fratelli tutti, 81).  Moyo wa shauku yao kwa hiyo Karadinali Parolini amesema ni kuitwa katika juhudi ya kuwa karibu na kukuza hadhi na  utu, kwa kuwa mashuhuda katika sehemu mbali mbali za maisha , kama vile mbegu ambazo kwa taratibi zinakuwa  zinachanua na kutoa matunda pamoja, hata ikiwa ndani ya kipindi ni kikavu kinaendelea na kubadilishana kwa dhoroba na upepo mkali.

Udugu wa Kibinadamu 10 Juni 2023
Udugu wa Kibinadamu 10 Juni 2023

Kardinali Parolin amesisitiza kwamba “Leo hii kuliko hapo awali katika ulimwengu wa haraka na mgumu tunaoishi, utandawazi mkubwa na ulichafuka zaidi, yote yanajiwakilisha kuunganishwa na kutegemeana, na hii ni sababu moja zaidi ya kukabiliana, kupanua mitazamo yetu  na kuunganisha nguvu, amekiri Katibu wa Vatican. Kwa hiyo akiendelea amefafanua kuwa Sababu ya amani inaomba, dharura kwa ajili ya ukosefu wa maendeleo ya haki inaombwa n azidi fungamani, nyumba ambayo wote wanaishi inaomba, katika ufahamu kwamba uchambuzi wa matatizo ya mazingira hauwezi kutenganishwa na uchambuzi wa binadamu, familia, kazi, mazingira ya mijini, na kutoka kwa uhusiano wa kila mtu na yeye binafsi (Fratelli tutti, 141).  Migogoro yote ambayo leo hii tunapitia, Kardinali Parolin amesema kiukweli ziwe za kisiasa za kijiografia, kazi, hali ya tabianchi, kijamii, zinashiriki hitaji la kushirikiana kwa faida ya wote, kujenga uhusiano, sheria na taasisi zenye uwezo wa kuangalia zaidi ya masilahi ya mtu binafsi: wanadai, kwa kusema, "ikolojia ya udugu wa wanadamu.

Historia yao na jitihada zao zinashuhudia kile ambacho kinawezekana; kushuhudaia ulimwengin katika wengi na katika mitindo mingi ambayo hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe (FT32;54;137).  Na leo hii, uwepo wao, wao wanathiminisha kuwa kujiachia kwenye ubinafais na mfuko inaezekana kuushinda na zaidi inapaswa kushindwa. Kwa kupyaisha shukurani za uwepo wao hapo, Kardinali Parolin ameashukuru kwa moyo na kuwatakia kazi nje. Kila lugha ambayo iliwakilishwa hapo na kukutana pamoja inaleta mlio wa neno la tumaini. Tumaini moja ambalo dunia inakiu, tumaini moja ambalo liwe la dhati, na tumaini ambao liwe na ujasiri.

Udugu wa kibinadamu
Udugu wa kibinadamu

Katika Tukio hilo la  Jumamosi tarehe 10 Juni 2023,  saa kumi jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kwa utashi wa Baba Mtakatifu lilizindua kwa upya ndoto yake ya Udugu na  pia kuwa na  fursa ya kumuombea  na kuwa karibu na Baba Mtakatifu Francisko ambaye amelazwa Hospitalini Gemelli. Takriban washindi 30 wa Tuzo ya Nobel walishiriki, katika Tukio la ‘Not Alone’ ambapo Carlo Conti wa Televisheni ya Italia aliwasilisha mashuhuda wa udugu na wasanii mbali mbali kama vile: Andrea Bocelli, Al Bano, Amara Roberto Bolle, Giovanni Caccamo, Cristicchi, Hauser, Carly Paoli,  Kwanya ya  watoto ya Antony, Mr. Rain, Amii Stewart na Paolo Vallesi, watakuwapo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Tukio la Udugu wa kibinadamu
Tukio la Udugu wa kibinadamu

Katika tukio hilo kubwa la kwanza kutanyika Viwanja 8 vingine duniani viliunganishwa kuanzia na: Brazzaville(Congo), Trapani (Mediterania Kuokoa Binadamu); Bangui (Jamhuri ya Afrika ya Kati); Ethiopia; Buenos Aires (Argentina); Yerusalemu(Israeli); Nagasaki(Japani); Lima(Peru). Mkutano huo ulikuwa mbashara kupitia Televisheni ya Vatican CTV Vyombo vya habari Vatican, mondo visione ya  Televisheni ya Italia (RAI1) kuanzia Jioni saa 11.00  - 12:45 na utitirishaji kwenye mtandao wa Fondazionefratellitutti.org na majukwaa yote ya Facebook na  YouTube ya Mfuko wa Fratelli tutti.

Kard Parolin katika Mkutano wa Udugu wa Kibinadamu
10 June 2023, 20:03