Tafuta

2023.06.07 Kimezinduliwa kituo cha Maelezo kwa ajili ya Jubilei ya 2025 kilichopo njia ya Conciliazione mita chache kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro. 2023.06.07 Kimezinduliwa kituo cha Maelezo kwa ajili ya Jubilei ya 2025 kilichopo njia ya Conciliazione mita chache kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro.  (Vatican Media)

Matashi mema kwa Papa kutoka kwa Kard.Parolin Katibu wa Vatican

Katibu wa Vatican,Kardinali Pietro Parolim amezindua kituo cha maelezo katika njia ya Conciliazione kwa ajili ya Jubilei 2025 na kujibu maswali ya waandishi wa habari juu ya upasuaji ambao Papa alikuwa akabiliane nao alasiri:Muda unaohitajika wa upasuaji lakini ni matumaini ya kuanza tena hata akiwa katika kitanda cha hospitalini kwa shughuli.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alielekeza  matashi mema kwa waandishi wa habari kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye alasiri alikuwa afanyiwe upasuaji tarehe 7 Juni 2023 katika hospitali ya Gemelli, Roma kwamba  "Tunamfuatilia kwa upendo wetu kwa maombi yetu tukitumaini kuwa kila kitu kitatatuliwa haraka iwezekanavyo." Hata hivyo mapema asubuhi habari hiyo ilitolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ambayo ilieleza kuwa: “ni Laparotomy na upasuaji wa plastiki wa ukuta wa tumbo na bandia chini ya anesthesia ya jumla, iliyoratibiwa na timu ya matibabu, ambayo itahitaji kukaa hospitali kwa siku kadhaa.” Alisema hayo katika fursa ya afla ya Uzinduzi wa kituo cha  maelezo ya Jubilei 2025.


Kardinali Parolin kwa njia hiyo majira ya saa 6 kamili hivi alizindua Kituo cha maelezo cha Jubilei 2025 mahali ambapo patakuwa  ni sehemu ya maelezo na mapokezi kwa ajili ya mahujaji wote watakaoshiriki  Jubilei inayofuata kwenye njia ya  Conciliazione, mita chache kutoka katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Katika fursa hiyo kwa sala na usomaji wa Injili, Kardinali Parolin akiwa pamoja na Askofu Mkuu Rino Fisichella, wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji alibariki jengo hilo ambalo tayari limeanza kufanya kazi kwa muda.

Kardinali alisali na kubariki jengo la Maelezo kwa ajili ya Jubilei 2025
Kardinali alisali na kubariki jengo la Maelezo kwa ajili ya Jubilei 2025

Akiwa  pembeni, ya afla hiyo alisimama  kidogo na wahandishi wa habari waliokuwepo kujibu maswali kuhusu upasuaji wa Papa, wa baada ya ule wa 2021 kwenye utumbo mpana. Alipoulizwa kama alikuwa na wasiwasi, Kadinali huyo alisema: “ Nisingejua la kusema, kwa sababu sina vipengele vyovyote vile. Hakuna cha kuongeza kwenye taarifa za vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican  ambayo, alisema, mambo kwa njia ya kiufundi sana akijaribu kutoa vipengele vinavyoruhusu tatizo la kupangwa vizuri. Akijibu swali jingine tena la mwandishi kuihusu shughuli: “ Hakuna uhamisho wa madaraka. Akiwa katika muda wa upasuaji huo, alieleza: “Nadhani itakuwa saa chache, muda muhimu wa upasuaji basi shughuli zitaanza tena, hata ikiwa ni kutoka kitanda cha hospitalini. Ikiwa kuna mambo ambayo yanahitaji kuamuliwa na ya haraka, yatapelekwa  kwake huko Gemelli”.

Baraka ya jengo hilo la maelezo ya Jubilei
Baraka ya jengo hilo la maelezo ya Jubilei

Katika mazungumzo mafupi ya Kardinali Parolin na waandishi wa habari, hakukosekana kurejea  suala la utume wa Kardinali Matteo Maria Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu Italia  (CEI) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna italia, huko Kyiv, nchini Ukraine, hatua ya kwanza ya utume aliyokabidhiwa na Baba Mtakatifu "ili kupunguza mvutano wa  kuteswa Ukraine. Kwa hiyo “Utume wa Kardinali Zuppi ulikusudiwa kama ushirikiano, mchango zaidi ambao Vatican inaweza pia kutoa kwa  ajili ya amani”, Kardinali Parolin alisisitiza.

Maji ya Baraka kubariki jengo la maelezo ya Jibilei 2025
Maji ya Baraka kubariki jengo la maelezo ya Jibilei 2025

Akiendelea na ufafanuzi huo alisema "Ninaamini kuwa hakuna jipya lililofanyika ikilinganishwa na yale ambayo Rais Zelensky alimweleza Papa wakati wa mkutano wao  mnamo tarehe 13, wakati kiongozi huyo wa Ukraine alipoomba msaada kutoka kwa Papa na Vatican ili kuwarudisha nyumbani watoto wa Ukraine walipelekwa nchini Urussi na Papa alipendekeza “Mfumo wetu wa Amani kama kanuni pekee ya ufanisi ya kufikia amani ya haki. Msimamo wa Ukraine siku zote ni sawa”, Kardinali Parolin alifafanua, “lakini ukweli wa kuzungumza na kusikia misimamo na mitazamo tofauti kidogo bila shaka unaweza kuwa wa manufaa na kupendelea amani. Na jinsi gani kutakuwa na maendeleo,  Sijui, itabidi tuone”, alisisitiza Kardinali.

Safari inayowezekana kwenda Moscow

Katika safari inayowezekana ya Kardinali Zuppi kwenda Moscow, Katibu wa Vatican alisema kwamba: “tutajadili naye (Kadinali Zuppi, ni hatua gani zaidi za kuchukua”. “Kwa upande wa Papa wazo lilizaliwa kama utume wa  kutekelezwa katika miji mikuu miwili, ambapo matarajio ya Moscow yanapaswa kubaki wazi, lakini kwa hakika tutaona”, alisema. Kwa sasa, mkutano kati ya Parolin na Zuppi umepangwa mara tu atakaporudi, basi bila shaka wataripoti kwa Papa.

Kardinali Parolin amtakia matashi mema Papa na pia kuzungumza juu ya utume wa Ukraine
07 June 2023, 18:28