Papa Francisko akabidhi kwa mama Maria vijana na hija yake
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kwa waandishi wa habari kutoka Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, tarehe 31 Julai 2023 inasema kuwa: “Leo mchana katika kesha la Ziara yake ya Kitume ijayo huko Ureno, katika fursa ya Siku ya Vijana Duniani, Papa Francisko amekwenda kama kawaida yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, mahali ambapo amekaa kwa sala mbele ya Picha ya Bikira Salus Populi Romani, akimkabidhi safari na mamia elfu ya vijana atakaokutana nao katika siku sijazo.
Kwa hiyo kwa mara nyingine tena, katika mkesha wa kuondoka kwake kuelekea Ureno asubuhi ya tarehe 2 Agosti, 2023 Papa Francisko hakukatisha utamaduni wake wa muda mrefu kuelekea katika Kikanisa hiki pendwa. Na hii ni mara yake ya 109 kwenda kusali hapo. Papa Francisko alikuwa ametembelea Salus Populi Romani kwa mara ya mwisho mnamo Juni 16, ili kushukuru kwa matokeo ya mafanikio ya upasuaji wa laparatomy katika Hospitali ya Gemelli. Pia katika hafla hiyo, Baba Mtakatifu alikaribishwa mlangoni na wakati wa kutoka kwa salamu ya upendo ya waamini waliokusanyika katika uwanja wa kanisa kuu hilo baada ya kutulia katika sala kwa muda mfupi, wakati akiketi kwenye kiti cha magurudumu, mbele ya Picha ya Bikira Afya ya Watu wa Roma
Mbali na usimamizi wa Mama Maria Baba Mtakatifu pia alikuwa amewaomba wamini kusimndikiza katika safari hiyo iliyokaribia kwa sala. Alifanya hivyo mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa ajili ya vijana wa kike na kiume ambao kutoka mabara matano watakusanyika Lisbon kwa tukio la ulimwengu. Kwa hiyo alisema:"Nawaomba mnisindikize kwa maombi yenu katika safari yangu ya Ureno, ambayo nitaifanya kuanzia Jumatano ijayo", alisema Papa Francisko, tarehe 30 Julai 2023.