Saints Peter and Paul Cathedral in Ulaanbaatar Saints Peter and Paul Cathedral in Ulaanbaatar  Tahariri

Papa nchini Mongolia,kwa sababu ndani ya Kanisa haijalishi idadi

Maneno ya Mtakatifu Paulo VI yanasaidia kuelewa sababu za safari ambayo Fransisko anakaribia kuifanya katika nchi ya Asia

ANDREA TORNIELLI

Papa Francisko anakaribia kuondoka kuelekea Mongolia, ziara ambayo “alitamani sana”, ambayo tayari ilikuwa katika ratiba ambazo hazikutimizwa za Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, baada ya uwepo wa wamisionari mwanzoni mwa miaka ya 1990 alipokuwa amefufua jumuiya ya Kikristo. Kitakachopokelewa kwa kukumbatiwa na Mrithi wa Petro katika moyo wa Asia ni Kanisa “dogo kwa idadi, lakini lililo hai katika imani, na kuu katika mapendo”. Francisko atakutana sio tu na Wakatoliki 1,500 wa nchi hiyo, lakini watu wote “wakuu” na “wenye busara” na tamaduni yao kuu ya kibuddha.

Kwa nini Papa anakwenda Mongolia? Kwa nini anajikita kwa siku tano za ajenda yake(siku mbili za kusafiri pamoja na kukaa huko siku tatu)kutembelea kikundi kidogo kama hicho cha Wakatoliki? Je, “masuala ya kisiasa” yanahusiana nayo kwa kufanya safari ya kwenda nchi inayopakana na Shirikisho la Urussi na Jamhuri ya Watu wa China? Kiukweli, motisha wa kuhiji katika vitongoji vya Asia haina maana ya “masuala ya kisiasa” na kwa hakika sio mtazamo wa Upapa wa Jorge Mario Bergoglio.

Siku ya Jumatatu tarehe 30 Novemba 1970, Mtakatifu Paulo wa VI alifunga safari ndefu akifika mpaka kwenye Visiwa vya Samoa katika Bahari ya Pasifiki. Wakati wa adhimisho la Misa katika kijiji cha Leulumoega Tuai, kwenye pwani ya kaskazini-magharibi ya kisiwa cha Upolu, Papa Montini aliweka kando “sisi" ya watukufu ambayo ilitumiwa na mapapa na kusema: “Sio ladha ya kusafiri au hata shauku  yoyote iliyonileta kwenu: Nimekuja kwa sababu sisi sote ni ndugu, au tuseme kwa sababu ninyi ni wanangu na binti zangu, na ni sawa kwamba, kama baba wa familia wa , Familia hii ambayo ni Kanisa Katoliki, nioneshe kila mtu kwamba anastahili upendo ulio sawa. Je! mnajua maana ya “Kanisa Katoliki”? Inamaanisha kwamba imeundwa kwa ajili ya ulimwengu mzima, kwamba imeundwa kwa ajili ya kila mtu, kwamba hakuna mahali popote ni mgeni: kila mtu, taifa lolote, kabila lake, umri wake au elimu, anapata nafasi ndani yake.”

Kanisa, ni mahali pa wote. Kanisa, mahali ambapo kipaumbele si idadi na ambapo hakuna mtu  aliye mgeni, lugha yoyote, utamaduni, watu au taifa analotoka. Ni Kanisa “para todos”, kwa wote, , neno ambalo Francisko alizungumza akiwa  huko Lisbon. Kabla ya mwezi mmoja baada ya Siku ya Vijana Duniani (WYD), Askofu wa Roma anarudi barabarani, akiwaambia “Kaka  na dada zake wa Kimongolia” kwamba “anafurahi kusafiri kuwa kati yenu kama ndugu wa wote.”

Taariri ya Dk Andrea Tornielli kuhusu Ziara ya Kitume ya Papa nchini Mongolia kwa wakristo wachache
28 August 2023, 14:38