Tafuta

Kardinali Pironio ni mmoja kati ya watakaotangazwa wenye heri wapya Kardinali Pironio ni mmoja kati ya watakaotangazwa wenye heri wapya 

Kardinali Pironio ni mmoja watakaotangazwa wenyeheri wapya

Kati ya miujiza iliyotambuliwa kwa maombezi ya watumishi wa Mungu,yupo Kardinali wa Argentina ambaye,aliwahi kuwa rais wa Baraza la Kipapa la Walei na muandaaji wa Siku za Vijana Duniani ambayo ilizaliwa kutokana na maono ya Mtakatifu Yohane Paulo II.fadhila za kishujaa za mtawa wa kiroganisti na waanzilishi wawili wa Mashirika ya Kitawa.

Na Angella Rwezaula,  Vatican.

Wakati wa Mkutano na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na Baba Mtakatifu, ametoa idhini ya Baraza hilo kuwatangaza wenyeheri  wafuatao, kufuatia na muujiza wa maombezi ya mtumishi wa Mungu Kardinali Eduardo Francesco Pironio, wa Kanisa Takatifu la Roma; alizaliwa huko Nueve de Julio (Argentina) tarehe 3 Desemba 1920 na kifo chake  Roma (Italia) itarehe 5 Februari 1998.  Kardinali kwa walio wengi walimfahamu kama "rafiki wa Mungu", kama askofu mkuu wa wakati huo wa Buenos Aires Jorge Mario Bergoglio alivyomfafanua. Kwa kila mtu, yeye ndiye aliyeunga mkono na kisha kuandaa Siku za Vijana Ulimwenguni, akitimiza matakwa mazito ya Mtakatifu Yohane Paulo II.

Aliendeleza wazo la Papa kuunganisha vijana wote ulimwenguni WYD

Kama mkuu wa Baraza la Kipapa aliendeleza wazo la Papa la mkusanyiko mkubwa ambao ungehusisha wavulana na wasichana kutoka ulimwenguni kote. Wazo dogo ambalo liliibuka baada ya muda na kuwa moja ya hafla kubwa zaidi ya Kanisa Katoliki: Siku ya Vijana Ulimwenguni. Kwa Pironio, mwanzo wa utumishi wake katika Curia pia ulilingana na ugunduzi wa uvimbe wa kibofu ambao ulisababisha, kwa mateso makubwa, hadi kifo chake huko Roma mnamo 5 Februari 1998. Mwili ulihamishiwa Argentina, kwenye patakatifu pa Marian huko Luján. , mahali pale pale alipopokea ubatizo na kuwekwa wakfu uaskofu. Amri kuhusu asili ya fadhila za kishujaa za kutangazwa mwenyeheri zilikuwa ni tarehe 18 Februari 2022.

Mtumishi wa Mungu Padre Giuseppe Marrazzo

Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Padre Giuseppe Marrazzo, Kuhani wa Shirika la Waroganisti wa Moyo wa Yesu; alizaliwa tarehe 5 Mei 1917 huko Mtakatifu Vito ya Normanni (Italia) na kifo chake tarehe  30 novemba 1992 huko Messina (Italia). Alikuwa wa Puglia akitoka katika familia maskini, tunamkumbuka hasa kwa  ajili ya utume wake huko Messina ambako alijitolea kwa namna ya pekee kuungamisha akifuata mfano wa Mtakatifu Leopoldo Mandić Mkapuchi wa Croatia.

Mtumishi wa Mungu Sr Eliswa

Kwa njia hiyo wengine ni Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Eliswa  wa Mwenyeheri Bikira Maria Zamanai aliitwa: Eliswa Vakayil), Mwanzilishi wa Shirika la Wakalmaenti wa  Tatu wasio na vitatu, na sasa ni Watawa wakalmeri wa Teresa; alizaliwa tarehe  15 Oktoba 1831 huko Ochanthuruth (India) katika familia inayojiweza na kuwa na msingi wa dinia  na alikufa tarehe 18 Julai 1913 huko Varapuzha (India); Hata hivyo  akiwa mjane alichagua maisha ya sala na upweke, alijitolea kuwatunza maskini na aliishi katika kibanda cha kawaida. Mnamo mwaka wa 1862, pamoja na Padre Mkarmeli wa Kiitaliano asiye na viatu, Leopoldo Beccaro, aliunda Shirika la kwanza  mahalia huko Kerala, Masista wa Wakarmeli wateresa, waliojitolea kwa ajili ya  elimu ya wasichana maskini na mayatima na kuwasaidia walioachwa na wahitaji. Pamoja na shughuli zake, Mama Eliswa alichangia kukuza ubinadamu na kiakili kwa wanawake katika muktadha changamano wa kijamii na kidini wa India mwanzoni mwa karne ya 19 na 20.

Mtumishi wa Mungu Sr. Naria Francesca Foresti

Na hatimaye fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Francesca Foresti (zamani aliitwa: Eleonora), Mwanzilishi wa  Shirika la Masisita Wafransiskani waabuduo katika sehemu mbali mbali za udugu; alizaliwa tarehe  17 Februari 1898 huko  Bologna (Italia) na alifariki mnamo tarehe  12 Novemba  1953  huko Ozzano Emilia (Italia).  Hata hivyo katika mipango hiyo ambauo haikuwa daima rahisi na mwishowe ikawa nzuri. Mnamo 1919, alishiriki shana na Padre Pio wazo la kujitolea kwa  ajili ya maisha ya tafakuri yaani ya ndani, kwa kukuza ibada maalum kwa Ekaristi. Alijitolea kwa ajili ya elimu ya vijana kwa mafundisho ya Katekisimu, akiwafundisha kuishi maisha ya utii huku akiheshimu uhuru wa kila mtu. Na afya mbaya, kutokana na matatizo ya moyo, ilisababisha kifo chake akiwa na umri wa miaka 55 tu.

Wenyeheri wapya
08 November 2023, 18:18