Tafuta

Maaskofu wa Congo DRC Maaskofu wa Congo DRC  (AFP or licensors)

Papa amemteuwa Padre Abel Liluala kuwa Askofu Mkuu wa Ponte-Noire

Mheshiwa Padre Abel Liluala,ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Paroki wa Kanisa Kuu na Makamu Hakimu wa Jimbo Kuu la Pointe-Noire ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu hilo.Askofu Mteule Abel Liluala,alizaliwa 23 Aprili 1964 huko Cabinda,Angola na alipewa daraja la Upadre tarehe 6 Februari 1994 kwa Jimbo kuu la Pointe-Noire.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko  tarehe 6 Januari 2024 amepoka barua ya kuomba kung’atuka katika shughuli za Kichungahji za Jimbo Kuu la Pointe-Noire, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC)iliyowakilishwa na Askofu Mkuu Miguel Ángel Olaverri  Arroniz, S.D.B. na wakati huo huo akamteua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu hilo  hilo Mheshimiwa sana,Padre Abel Liluala, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Paroko wa Kanisa Kuu na Makamu Hakimu wa Jimbo Kuu la Pointe-Noire.

Wasifu wa maisha

Askofu Mkuu Mteule Abel Liluala, alizaliwa 23 Aprili  1964 huko Cabinda, Angola, karibu na Pointe-Noire. Baada ya Seminari Ndogo ya Tshela, katika Jimbo la Boma, alipata mafunzo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu André Kaggwa huko Kinshasa DRC. Alisoma Taalimungu katika Seminari Kuu ya Moyo Mtakatifu huko Luanda, Angola na baadaye katika Seminari Kuu ya Emile Biayenda huko Brazzaville.

Alipewa daraja la Upadre tarehe 6 Februari 1994 kwa Jimbo kuu la Pointe-Noire. Mwaka 2010 alipata shahada ya udaktari katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu(Santa Croce) jijini Roma. Pia alikuwa mwanachama wa Chuo cha Washauri cha Pointe-Noire. Hadi uteuzi huo  kwa hiyo alikuwa ni Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Mtume na Makamu katika Mahakama ya Jimbo Kuu la Pointe-Noire.

Askofu Mkuu Mpya wa Ponte Noire (DRC)
08 January 2024, 11:34