Tafuta

Misa ya Siku ya Wazee dunaini tarehe 23 Julai 2023 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu petro mjini Vatican. Misa ya Siku ya Wazee dunaini tarehe 23 Julai 2023 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu petro mjini Vatican.   (Vatican Media)

'Katika uzee wangu usiniache' ni mada ya Siku ya IV ya Babu/bibi na Wazee duniani 2024

Dominika tarehe 28 Julai 2024 itaadhimishwa Siku ya IV ya Babu/bibi na Wazee duniani.Kauli mbiu iliyochaguliwa na Papa ni:“Katika uzee wangu usiniache”(Zab71,9).Ni mada inayotaka kusisitiza jinsi upweke kwa bahati mbaya ni mchungu ukisindikiza maisha ya wazee wengi na mara nyingi ni waathiriwa wa utamaduni wa kubagua.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 15 Februari 2024, Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha, ametoa kauli mbiu iliyochaguliwa kwa Siku ya IV ya Babu/bibi na Wazee. Katika taarifa yake amesema kuw:  “Dominika tarehe 28 Julai 2024 itaadhimishwa Siku ya IV ya Babu/bibi na Wazee Ulimwenguni. Kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu ni “ Katika uzee wangu usiniache”(Zab71,9), ambayo inataka kusisitiza jinsi ambavyo upweke kwa bahati mbaya ni mchungu ukisindikiza maisha ya wazee wengi na mara nyingi,ni waathiriwa wa utamaduni wa kubagua.”

Wazee wakati wa siku ya wazee 2023
Wazee wakati wa siku ya wazee 2023

Katika taarifa hiyo aidha inabanisha kuwa: “Katika mwaka wa maandalizi ya Jubilei ambayo Baba Mtakatifu amechagua kujikita kwa sala, Kauli mbiu ya Siku hii imetolewa katika Zaburi ya 71 ambayo ni sala ya mzee anayepitia  historia yake ya urafiki na Mungu.” Kwa mujibu wa Kardinali Kevin Farrell,  amesisitiza kuwa: “Maadhimisho ya Siku,  haya yanathamanisha karama za babu/ bibi na Wazee na uhusiano wao na maisha ya Kanisa, ambayo inataka kusaidia jitihada za kila Jumuiya ya Kanisa katika kujenga uhusiano kati ya kizazi na kupambana na upweke kwa utambuzi kuwa kama maandiko yanavyothibitisha: “  Sivizuri binadamu kuishi peke yake”(Mw 2,18).

Kauli mbiu ya Siku ya wazee ulimwenguni ni "katika uzee wangu usiniache"
15 February 2024, 15:31