2024.02.09 Kardinali Czerny  amebariki Mtumbwi kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi huko Sudan Kusini. 2024.02.09 Kardinali Czerny amebariki Mtumbwi kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi huko Sudan Kusini.  (© X - VaticanIHD)

Kard.Czerny abariki mtumbwi kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu,katika siku yake ya mwisho wa safari nchini Sudan Kusini alibariki Mtumbwi uliopewa jina la Josephine Bakhita,Mtakatifu msimamizi wa waathirika wa watumwa.Caritas itautumia kupeleka wakimbizi wa Sudan kwa kusaidia kukatisha Mto Nile.

Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula - Vatican.

Katika siku yake ya mwisho wa safari nchini Sudan Kusini, aliyoianza tarehe 2 hadi 9 Februari 2024, Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungani ya Binadamu, Ijumaa tarehe 9 Februari alibariki Mtumbwi kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi wote wanaolazimika kuvuka mto Nile nchini  Sudan.

Mtumbwi/Boti kwa ajili ya wakimbizi
Mtumbwi/Boti kwa ajili ya wakimbizi

Mtumbwi huo umepewa jina la Josephine Bakhita, kama Mtakatifu kutoka Darfur ,Sudan Kusini ambaye alikuwa mtumwa na anayeheshimiwa kama mlinzi wa waathiriwa wote wa utumwa wa zamani  na wa  mbamboleo. Caritas Eneo itakuwa na jukumu la kuutumia mtumbwi huo wa mbao na chuma kuwasafirisha wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi jirani ya Sudan, iliyoharibiwa na mzozo kwa miezi kumi iliyopita ambao umesababisha dharura ya kibinadamu ya idadi kubwa na watu milioni 25, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, na ambao wanaohitaji msaada na ulinzi.

Maji ya amani

Mtumbwi huo utasaidia watu wanaokimbia nchi kuvuka njia kubwa ya maji, ambapo kuna hatari na vikwazo vingi, kuanzia mpaka wa Renk hadi huko Malakal. “Utakuwa Mtumbwi ambao utaacha nyuma dhoruba ya migogoro, vurugu, chuki na manung'uniko na utasafiri katika maji yenye amani zaidi ambapo watu wanaweza kuishi pamoja kama kaka na dada," alisisitiza Kardinali Czerny, bila kuficha hisia zake, wakati wa afla hiyo kwenye bandari ya Juba.  Kwa njia hiyo hicho kilikuwa kitendo cha mwisho wa safari iliyoanza  mnamo Februari 2 iliyopita ili kuzindua upya ombi la Papa la amani, mwaka mmoja baada ya hija ya kiekumene ambayo Baba Mtakatifu  alitaka kutekeleza katika ardhi hiyo iliyojeruhiwa akiwa  bega kwa bega na Mkuu wa Kianglikani Askofu Mkuu Justin Welby na Msimamizi Mkuu  wa Kanisa la Scotland, Ian Greenshields.


Ziara za Renk na Malakal

Hatua mbalimbali ziliashiria safari Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Safari kwa njia hiyo ya ilikuwa Malakal kwa ajili ya Misa Takatifu katika fursa ya Mtakatifu Josephine Bakhita, sanjari na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Biashara Haramu wa Binadamu, ambapo Kardinali alisisitiza na kuonya juu ya “miungu” au “sanamu” za uwongo, kama vile uroho wa pesa na uchu wa madaraka, njaa ya kutawala na kutawaliwa, kutengwa kwa sababu ya uzalendo, utaifa na ukabila, ambao hadi leo hii unaharibu maisha ya wengine na ambao umeiharibu Sudan Kusini yenyewe.”

Kardinali Czerny akibariki Mtumbwi
Kardinali Czerny akibariki Mtumbwi

Huko Malakal, pia Kardinali Czerny aliweza kuona na kuthamini kazi ya makaribisho yanayofanywa na Jimbo hilo na jumuiya ya eneo hilo, licha ya ukweli kwamba rasilimali za ndani ni chache. Huko Renk, Kadinali Czerny alitembelea eneo la mapokezi la wahamiaji na wakimbizi wa Sudan. Kwa hiyo, katika mji mkuu Juba, ambapo Dominika tarehe 4 Februari 2024 aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa, na hivyo alitaka kuthibitisha tena hija hiyo katika nyayo za Papa kwa ishara ya umakini mkubwa wa Kanisa kuelekea dharura  ambazo mara nyingi, zinaongeza uhamiaji.

Kardinali Czerny amebariki Mtumbwi kwa ajili ya wahamiaji nchini Sudan
10 February 2024, 09:15