Nchi Takatifu,Kard.Parolin:hasira kwa mauaji,ujasiri unahitajika kwa suluhisho
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican amenukuu maneno ya Mtakatifu Augustino ili kutoa maoni yake juu ya hali ya Mashariki ya Kati, hasa huko Gaza, ambapo kwa vifo elfu 30 kuna kile alichofafanua kama mauaji na pia kuomba suluhisho la haraka. Kardinali akiwa anaongoza ujumbe wa Vatican alasiri Jumanne , tarehe 13 Februari 2024, kwa ajili ya mkutano wa kiutamaduni wa nchi mbili ili kuadhimisha kumbu kumbu ya Mkataba wa Lateran, ambao sasa unaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake, mwishoni mwa mkutano ambao ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella na Waziri Mkuu Giorgia Meloni, alielezea hali ya Nchi Takatifu.
Kardinali lieleza juu ya upande mmoja, dharau na kwa upande mwingine, tumaini, akijibu maswali ya waandishi wa habari, pembeni mwa mkutano huo huko akiorodhesha mada zilizojadiliwa katika mazungumzo marefu nyuma ya milango iliyofungwa ikiwa ni pamoja na mwisho wa maisha, sera za familia na kuthamini posho moja, Imu, Jubilee na, bila shaka, migogoro inayoikumba dunia hii. “Pamoja na Rais wa Jamhuri na pia na Waziri wa Mambo ya Nje, muhtasari ulitolewa wa hali zote za shida ambazo kwa sasa zinasumbua ulimwengu na kuna hata wasiwasi kwa upande wa Italia na Vatican alielezea Kardinali. “Ni vigumu zaidi kupata ufumbuzi wa matatizo haya, lakini tunajaribu kutoa mchango ambao unaweza kuwa chanya na kuanzisha njia za kuelekea amani.”
Waziri wa Mambo ya Nje mwenyewe, Antonio Tajani, tarehe 13 Februari alizungumza kuhusu mwitikio usio na uwiano kwa upande wa Israel katika Ukanda huo. Italia, kwa hivyo, inaonekana kuungana na kile, ambacho Kardinali Parolin alisema, “sauti ya jumla na kwamba hatuwezi kuendelea hivi. Tunahitaji kutafuta njia nyingine za kutatua tatizo la Gaza, tatizo la Palestina” - alisema Waziri wa Mambo ya Nje -. Vatican imesema tangu mwanzo: kwa upande mmoja, hukumu ya wazi na isiyozuiliwa ya kile kilichotokea tarehe 7 Oktoba, na ninarudia hapa; hukumu ya wazi na isiyozuiliwa ya kila aina ya chuki dhidi ya Wayahudi, na ninairudia hapa. Lakini wakati huo huo pia ombi kwamba haki ya utetezi ya Israeli ambayo ilitolewa ili kuhalalisha operesheni hii ilingane na kwa hakika na vifo elfu 30 hailingani. Suluhisho la mzozo kwa sasa linaonekana kuwa mbali, lakini, Parolin alisema, "lazima tusikate tamaa. Mtakatifu Augustino alisema matumaini yanatokana na hasira na ujasiri, naamini sote tunakerwa na tukio hili la mauaji lakini tuwe na ujasiri wa kusonga mbele na tusikate tamaa kwani tukipoteza matumaini tunakumbana na mkono. Badala yake tunahitaji kupigana hadi mwisho na kujaribu kutoa mchango wetu, mchango wetu kadri tuwezavyo."
Akihimizwa na waandishi wa habari, kadinali huyo kisha akatoa taarifa kuhusu matokeo ya mkutano wa nchi hizo mbili na serikali: "Ilienda vizuri sana, kwetu sisi katika ujumbe wa Vatican na nadhani pia kwa wajumbe wa Italia ulikuwa mkutano mzuri sana, tuliweza kugusa baadhi ya masuala na mengine hata kuyachunguza kwa undani zaidi." Zaidi ya mada zote za "Kiitaliano", alisema: familia na masharti ya familia, kwa kutambua kile ambacho serikali imefanya kama posho moja kwa watoto, lakini bila shaka kuna nafasi ya kuingilia kati." Kisha mada ya shule za kibinafsi na pia mwisho wa maisha. Kuhusu suala hilo la mwisho, Kadinali huyo alieleza: "Tumegundua kwamba mikoa inajaribu kukabiliana na ukosefu huu wa sheria kwa upande wa Italia kwa matatizo ya aina hii lakini hakuna ufumbuzi". Suala la IMU pia liko mezani, katika suala hilo pia Parolin alisema: "Hapa sio suala la kufikia hitimisho lolote. Tukio la Makubaliano ya Lateran ni zaidi ya kitu kingine chochote wakati ambapo hali hiyo inazingatiwa. Jambo zuri ni utayari wa kushirikiana na kufuatilia masuala haya."