Tafuta

2024.02.12 S.E. Bwana Javier Gerardo Milei, Rais wa Jamhuri ya Argentina. 2024.02.12 S.E. Bwana Javier Gerardo Milei, Rais wa Jamhuri ya Argentina.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amekutana na Bw,Mleli, Rais wa Jamhuri ya Argentina

Baba Mtakatifu Francisko Februari 12,2024 amekutana na Rais wa Jamhuri ya Argentina,Bwana Javier Gerardo Milei.Mara baada ya Mkutano huo amekutana na Kardinali Paroli,Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko asubuhi tarehe 12 Februari 2024, amekutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, na Rais wa Jamhuri ya Argentina, Bwana Javier Gerardo Milei, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu  wa Vatican,  wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Wakati wa mazungumzo yao ya  ukarimu katika Sekretarieti ya Vatican wameonesha kuridhika na mahusiano mazuri yaliyopo  kati ya Vatican na Jamhuri ya Argentina na hamu ya kuyaimarisha zaidi. Na baada wakazingazia mpango mpya wa Serikali wa kukabiliana na msukosuko wa kiuchumi.

Papa Francisko na Rais na ujumbe wake kutoka Argentina
Papa Francisko na Rais na ujumbe wake kutoka Argentina

Wakati wakiendelea na mazungumzo yao, baadhi ya masuala ya kimataifa yaliguswa, hususan migogoro inayoendelea na kujitolea kwa amani kati ya mataifa. Katika mazungumo  hayo vile vile wamegusia mada zenye tabia ya Kimataifa kwa namna ya pekee migogoro inayoendelea na jitihasa kwa ajili ya amani kati ya mataifa.

Rais wa Argentina wakati wa kuzungumza na Sekretatieti ya Vatican
Rais wa Argentina wakati wa kuzungumza na Sekretatieti ya Vatican

Zawadi kutoka kwa Baba Mtakatifu: Medali ya shaba iliyochochewa na kifuniko cha Altare ya Mtakatifu Petro. Idadi ya hati za upapa na Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2024.

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi

Zawadi kutoka kwa Rais: Ishara  ya posta iliyowekwa na Ofisi ya Posta ya Argentina kwa ajili ya Mama Antula ambaye ametangaza kuwa mtakatifu tarehe 11 Februari 2024. Nakala ya hati ambayo Serikali ya Argentina iliidhinisha ya Juan Bautista Alberdi kama Mkataba wa makubaliano ya Papa (1854) na hatimaye baadhi ya keki za kawaida za Argentina.

Rais wa Argentina akisindikizwa kuonana na Papa
Rais wa Argentina akisindikizwa kuonana na Papa
12 February 2024, 15:56