Papa Francisko akutana na Waziri Mkuu wa Romania
Na Angella Rwezaula‘- Vatican
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, imebanisha kuwa Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 15 Februari 2024 amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Romania, Bwana Ion-Marcel Ciolacu ambaye mara baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.
Wakati wa mazungumzo yao na Sekretarieti ya Vatican wamesisitiza juu ya kuongezeka kwa hali ya juu ya mahusiano mazuri kati ya Vatican na Romania na juu ya mitindo ya ushirikiano wa juu katika sehemu zote mbili kwa ajili ya manufaa ya watu wa Romania hasa katika muktadaha wa Elimu. Baadaye, baadhi ya mada za maslahi ya pande zote na masuala ya sasa yaligusiwa ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Israeli na Palestina na Ukraine, kupokea wahamiaji na wakimbizi, pamoja na matarajio ya upanuzi wa mpango wa Ulaya.
Katika kubadilishana zawadi, Baba Mtakatifu Francisko amempatia waziri Picha ya shaba inayoleza ‘Ukaribu’; Idadi ya hati za upapa; Ujumbe wa Amani wa mwaka 2024 na Kitabu kuhusu Statio Orbis cha tarehe 27 Machi, 2020 kilichohaririwa na LEV. Kitabu cha Nyumba ya Kipapa ya Mikutano, iliyohaririwa na Mkuu wa Nyumba ya Kipapa. Wakati huo huo, Wziri Mkuu amemzawadia Papa Mchoro unaoonesha maaskofu saba wafiadini waliotangazwa kuwa wenyeheri na Papa Francisko mnamo mwaka wa 2019.