Tafuta

Televisheni ya Italia (Rai; Imewawakilishi kipindi 'Davanti alla Porta Santa'-"Mbele ya Mlango Mtakatifu",kama sehemu ya Mpango wa maandalizi ya Jubilei 2025. Televisheni ya Italia (Rai; Imewawakilishi kipindi 'Davanti alla Porta Santa'-"Mbele ya Mlango Mtakatifu",kama sehemu ya Mpango wa maandalizi ya Jubilei 2025.  (ANSA)

Safari kuelekea Jubilei na vipindi vya kila Juma vya RAI 1

"Mbele ya Mlango Mtakatifu"ni tukio la kwanza la Kipindi cha televisheni,kuanzia Dominika tarehe 25 Februari 2024 ambacho kupitia Televisheni ya Taifa Italia(Rai)itaendesha kama sehemu ya kusimulia historia ya Mwaka Mtakatifu 2025,ambao tayari umeanza na mwaka wa Sala kwa utashi wa Papa Francisko.

Vatican News

Huduma, mahojiano na ripoti zitarejea historia yake lakini pia zitapendekeza safari katika ulimwengu wa kisasa, miongoni mwa vijana na sehemu mbalimbali, nchini Italia na nje ya nchi, ili kusimulia historia  na kutoa sauti kwa mahujaji. Imetayarishwa na Televeshini ya Italia (Rai) ya Vatican, ambapo matangazo ya Kipindi hicho  yaliwasilishwa Alhamisi tarehe 22 Februari 2024  katika mkutano na waandishi wa habari.

Uwakilishi wa Kipindi kuhusu Jubilei 2025 katika Televisheni ya Italia
Uwakilishi wa Kipindi kuhusu Jubilei 2025 katika Televisheni ya Italia

Kipindi cha kwanza kilitayarishwa “Mbele ya Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro,” ambacho kitatambulisha historia yake na kitahusu Jubilei za karne zilizopita. Ripoti itafuatilia wasifu wa hija, wakati kwa mtazamo wa kimataifa kwa kujaribu kuelewa wapi mahali pa kupata tumaini leo hii. Mgeni mkuu atakuwa Askofu Mkuu  Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Uinjilishaji.

Jubilei 2025 Mahujaji wa Matumaini

“jarida la kila Juma linalotayarishwa na Rai -Vatican na kusimamiwa na mkurugenzi wake Stefano Ziantoni, litatangazwa kuanzia Dominika tarehe 25 Februari 2024 wakati wa kipindi cha Rai1, saa 6.45 za usiku, na litapatikana kwenye Rai Play. Litatoa ushuhuda, mahojiano, huduma za kiutamaduni, ili kuwaambia wadadisi na kuanzia Septemba ijayo litakuwa tukio la kila siku. Matangazo hayo, yaliyowasilishwa tarehe 22 Februari 2024  jijini Roma katika mkutano na waandishi wa habari, yataturuhusu kukaribia Jubilei pia kupitia simulizi kutoka ulimwenguni, yatatoa sauti kwa mahujaji, yatachunguza katika mwaka huu wa maandalizi yaliyowekwa kwa ajili ya  sala,  kwa Utashi wa Papa Francisko,  jinsi ya kusali katika mahali patakatifu, katika magereza, katika nyumba za watawa na watajaribu kuelewa jinsi gani vijana wanasali na kuna uhusiano gani kati ya sala na Akili Mnemba.

Jubilei pia ni utamaduni

Askofu Mkuu Fisichella alifafanua kuwa: “Uzalishaji wa awali na wa ubunifu, haifuatilii mifumo iliyojulikana tayari, lakini inatoa mwelekeo wa matarajio. Mpango ambao una ufunguzi wa kiutamaduni muhimu, kwa kuwa “Yubile ni utamaduni.” Mwenyekiti wa Uinjilishaji pia  alisisitiza kwamba “taarifa za jumla ni za msaada mkubwa hasa kwa vikundi vya watu wachache ambavyo havina uwezekano mwingi wa kuhisi umoja katika imani”, akiongeza kusema jinsi ambavyo ukumu la vyombo vya habari ni muhimu leo hii. Akizungumza kwa vyombo vya habari vya Vatican , Askofu  Mkuu Fisichella aliakisi jinsi ambavyo “kusubiri kuvuka Mlango Mtakatifu kunahitaji maandalizi ya kutosha, kwa sababu hiyo Papa Francisko alitaka kutanguliza Jubilei kwa mwaka wa sala, ili Mlango huo uweze kuakisiwa  kwa maana ya ndani zaidi.”

Uwakilishi wa Kipindi cha Jubilei 2025 katika RAI 1
Uwakilishi wa Kipindi cha Jubilei 2025 katika RAI 1

Na kuhusu mchango ambao vyombo vya habari vinaweza kutoa, alieleza kuwa “ni chombo chenye maamuzi na kwa hiyo hawana uwezo wa kutoa habari tu, bali pia kuwasiliana na mahujaji, ambao kwa njia ya mawasiliano wanakuwa wahusika wakuu kwa sababu sio tu kwamba wanaweza kusimulia hisotria zao  kwa wengine, lakini pia wanaweza kuwafanya waelewe thamani kubwa ya hija zao.

Programu ya ulimwengu

Jubilei 2025 ya Mhujaji wa Matumaini itakuwa  kwa hiyo kipindi cha “kidunia” kwa mujibu  wa  mkurugenzi wa Rai - Vaticano, Stefano Ziantoni  na kwamba  inazungumza na kila mtu, na ambayo itahusisha sana vijana, washawishi.” Kipindi cha kwanza kitarejea wakati, hadi kwenye habari fulani za kwanza za Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Vatican iliyoanzia mnamo mwaka 1500, kwa Papa wa wakati ule  Alexander VI, lakini pia itakumbusha baadhi ya maandiko ya kihistoria ambayo yanataja mlango uliofunguliwa katika Jubilei  ya 1350 pamoja na Papa  Clement VI na katika 'Mwaka Mtakatifu wa 1423, na pengine ule wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano.

Askofu Mkuu Fisichella akizungumza na Stefano Ziantoni Mhusika wa Rai - Vatican wakati wa uwakilishi wa kipindi cha Jubilei
Askofu Mkuu Fisichella akizungumza na Stefano Ziantoni Mhusika wa Rai - Vatican wakati wa uwakilishi wa kipindi cha Jubilei

“Kisha tutapiga hatua katika ulimwengu wa leo hii, tukiwa na maoni na matarajio ya watu kuhusu mwaka wa Jubilei. Mkuu wa Rai -Vatican alifafanua kwamba bidhaa ya televisheni ya haraka na yenye nguvu iliundwa, kijana, isiyochosha, inayotoa historia mpya na pia udadisi. Kwa hivyo, kwa mfano, “katika sehemu ya pili tutasikiliza historia ya mchongaji pekee aliye hai aliyeunda Mlango Mtakatifu, ule wa Mtakatifu Maria Mkuu,” na katika sehemu ya tatu tutakwenda, pamoja na Klabu ya Alpine ya Italia(CAI) ili kugundua misalaba 14 ya Jubilei iliyotangazwa  na Papa Leo XIII katika vilele vingi." Alisisitiza mhusika huyo

Hata hivyo akiendelea na maelezo alisema kuwa "Kamera za Rai pia ziliingia kwenye kiwanda ambacho Mlango Mtakatifu, wa Mtakatifu Petro ulitengenezwa na kwa, Mfuko wa Mazingira wa Italia (FAI), zitaonesha maeneo yanayojulikana na yasiyojulikana sana, kama vile “ambapo koti la silaha ambalo waliweka juu ya mkate kwa ajili ya ushirika wa watu wa Byzantine”. Haya yote, yanaruhusu kuchanganya utamaduni, mazingira, historia na mengi zaidi,” alihitimisha Ziantoni.

Mpango wa Vatican na RAI kwa ajili ya Jubilei 2025
23 February 2024, 12:01