Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
PROGRAMU YA KISWAHILI
Ratiba Podcast
Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Jacques Assanvo Ahiwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe. Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Jacques Assanvo Ahiwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe. 

Askofu Mkuu Jacques Assanvo Ahiwa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe

Askofu mkuu mteule Jacques Assanvo Ahiwa alizaliwa tarehe 6 Januari 1969 huko Jimbo kuu la Abidjani, Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 13 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Grand-Bassam. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 5 Mei 2020 akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe na hatimaye, akawekwa wakfu kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 25 Julai 2024 amemteuwa Askofu Jacques Assanvo Ahiwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe “Côte d’Ivoire.” Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Jacques Assanvo Ahiwa alikuwa ni Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké. Askofu mkuu mteule Jacques Assanvo Ahiwa alizaliwa tarehe 6 Januari 1969 huko Jimbo kuu la Abidjani, Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 13 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Grand-Bassam.

Pwani ya Pembe kuna ongezeko kubwa la miito  mitakatifu
Pwani ya Pembe kuna ongezeko kubwa la miito mitakatifu

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 5 Mei 2020 akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe na hatimaye, akawekwa wakfu kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké. Tarehe 16 Februari 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo kuu la Bouaké. Na ilipogota tarehe 25 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe “Côte d’Ivoire.” Anatarajiwa kusimikwa rasmi tarehe 14 Septemba 2024.

Uteuzi Pwani ya Pembe
26 Julai 2024, 15:12
Prev
February 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
232425262728 
Next
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031