Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Rondeaux: Allegro
Ratiba Podcast
Papa amemteua Monsinyo John Joseph Kennedy kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi. Papa amemteua Monsinyo John Joseph Kennedy kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi.  

Askofu Mkuu John Joseph Kennedy Katibu Mkuu, Idara ya Nidhamu

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 29 Julai 2024 alimteuwa Monsinyo John Joseph Kennedy kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi. Askofu mteule alizaliwa tarehe 15 Julai 1968. Daraja Takatifu ya Upadre akapewa tarehe 13 Julai 1993. Mwaka 2003 akateuliwa kuwa Afisa. Na mwaka 2017 akateuliwa kuwa Mkuu wa Idara 2022 Katibu Mkuu; 2024 Askofu mkuu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 29 Julai 2024 alimteuwa Monsinyo John Joseph Kennedy kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi. Askofu mkuu mteule John Joseph Kennedy alizaliwa tarehe 15 Julai 1968 huko Jimbo kuu la Dublin, nchini Ireland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Julai 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu, Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma.

Askofu mkuu John Joseph Kennedy, Katibu mkuu Idara ya Nidhamu
Askofu mkuu John Joseph Kennedy, Katibu mkuu Idara ya Nidhamu

Kuanzia mwaka 2003 aliteuliwa kuwa ni Afisa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Na tangu Mwaka 2017 akateuliwa kuwa ni Afrisa Mwandamizi Idara ya Nidhamu, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Tarehe 23 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na tarehe 29 Julai 2024 akampandisha hadhi na hivyo kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi.

Uteuzi
01 Agosti 2024, 14:52
Prev
February 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
232425262728 
Next
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031