Papa amemteua Sr.Inês,A.S.C.,kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Shirika la Kimisionari la Utoto Mtakatifu
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024 amemteua Katibu Mkuu mpya wa shughuli za Kipapa za Shirika la Kimisionari la Utoto Mtakatifu, Mhemishwa Sr. Inês Paulo Albino,A.S.C.,ambaye hadi uteuzi alikuwa ni Mshauri wa Shirika la Masisita Waabuduo wa Damu Takatifu.
Wasifu wake
Sr. Ines Paulo Albino, alizaliwa tarehe 25 Aprili 1969 huko Bula(Guinea-Bissau) na alifunga nadhiri za daima katika Taasisi ya Waabuduo wa Damu Takatifu mnamo tarehe 4 Septemba 1997. Aliendelea na masomo na kupata leseni ya Taalimungu ya Biblia katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma. Tayari alikuwa ni mhusika wa kichungaji wa Parokia ya Mtakatifu Maria de Mattias huko Ingoré na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kitaifa ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa huko Bissau. Alijikita kwenye nyanja za uinjilishaji, wa katekesi, ufundishaji na utume wa vijana. Mnamo 2022 amekuwa Mshauri na Mchumi wa Kanda ya Italia Shirika hilo la kitawa.