Tafuta

2024.08.22 Papa amepkea Barua na Hati za Utambulisho wa Bwana Juraj Priputen,Balozi wa Jamhuri ya Slovakia. 2024.08.22 Papa amepkea Barua na Hati za Utambulisho wa Bwana Juraj Priputen,Balozi wa Jamhuri ya Slovakia.  (Vatican Media)

Papa apokea Barua na Hati za Utambulisho wa balozi wa Slovakia

Bwana Juraj Priputen Balozi Jamhuri ya Slovakia mewakilisha Barua na hati za Utambulisho kwa Papa Francisko mjini Vatican tarehe 22 Agosti 2024.Alizaliwa tarehe 18 Julai 1975 huko Bratislava,ameoa na familia ya watoto wawili.Elimu ya mafunzo,Shahada na Shahada ya Uzamili kutoka Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa huko Moscow.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 22 Agosti 2024, Baba Mtakatifu Francisko amepokea Hati na barua za Utambulisho kutokakwa  Bwana Juraj Priputen, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia akiwakilisha Nchi yake  mjini Vatican. Bwana Juraj Priputen alizaliwa tarehe 18 Julai 1975 huko Bratislava, ameona na kuwa na familia ya  watoto wawili. Elimu ya mafunzo, ni pamoja na kupata  Shahada na Shahada ya Uzamili kutoka Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa huko Moscow, Kitivo cha Haki za Kimataifa (1992 – 1997) na Udaktari katika Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Comenius huko Bratislava (1999 – 2000) na ambacho  ni chuo kikuu cha kisasa cha Ulaya kilichoanzishwa miaka zaidi ya 105 iliyopita.

Papa amepokea barua na hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Slovakia
Papa amepokea barua na hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Slovakia

Vile vile Balozi huyo amefunika nyadhfa mbali mbali kama vile: Afisa wa Dawati, Idara ya Haki za Kibinadamu, Idara ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, MAE (1997 - 2000),  Mshauri wa Haki za Kibinadamu, Ujumbe wa Kudumu wa Jamhuri ya Slovakia katika Umoja wa Mataifa, New York (2000 - 2004), Mkurugenzi wa Ofisi ya Katibu Mkuu, MAE (2004 – 2006), Naibu Mkuu wa Balozi, Ubalozi katika Shirikisho la Urusi (2006 - 2010), Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Mkurugenzi Mkuu wa Rasilimali Watu na Naibu Katibu Mkuu, MFA (2010 - 2013), Balozi wa Kroatia (2013 - 2018), Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Kibinadamu, MAE (2018 - 2019), Mshauri wa Sera ya Kigeni kwa Rais wa Baraza la Kitaifa la Jamhuri ya Slovakia (2019 - 2024).

Barua na utambulisho wa Balozi wa Slovakia
22 August 2024, 14:55