Tafuta

Kupakia vyakula kwa ajili ya kupeleka huko Ukraine. Kupakia vyakula kwa ajili ya kupeleka huko Ukraine. 

Papa anaendelea na upendo kwa Ukraine:vifurushi vya chakula na dawa katika maeneo ya vita

Malori yenye nguo,madawa,chakula hasa tuna kwa ajili ya watu wanaoteseka kutokea Basilika ya Kiukraine ya Hagia Sophia huko Roma yameondoka tarehe 7 Agosti 2024.Huu ni msaada kwa ajili ya usambazaji uliokabidhiwa kutoka Baraza la Kipapa la Upendo.

Vatican News

Hatua ya Papa ya upendo kuelekea Ukraine, ambayo imekuwa ikifafanuliwa kama nchi ya ‘kuteswa’, inaendelea pia katika msimu wa joto. Kama ilivyokuwa katika miezi iliyopita, malori yenye chakula, nguo na madawa kwa ajili ya watu wanaoteseka katika nchi ya Ulaya Mashariki yameondoka Jumatano tarehe 7 Agosti 2024 kutokea katika  Basilika ya Kiukreni ya Hagia Sophia huko Roma. Hasa, wakati huu masanduku yenye tuna na chakula cha muda mrefu.

Ishara ya kuonesha ukaribu wa kibaba

Kwa mara nyingine tena, Ofisi ya Baraza la Kipapa la Upendo  linaloongozwa na  Kardinali Konrad Krajewski, ndiyo lenye dhamana ya kutuma na kusambaza zawadi hizi kutoka kwa Baba Mtakatifu kwenda Ukraine. Ishara mpya ya kusisitiza ukaribu wake na nchi, ambayo hata leo, mwishoni mwa hadhara kuu, aliomba sala na ukaribu kutoka kwa waamini wote.

Papa atuma msaada mwingine Ukraine
07 August 2024, 17:05