Tafuta

2024.10.17 Matembezi ya mawaziri kwa ajili ya ulemavu wa G7 katika makumbusho ya Radio Vatican. 2024.10.17 Matembezi ya mawaziri kwa ajili ya ulemavu wa G7 katika makumbusho ya Radio Vatican.  

G7:Mawaziri kwa ajili ya ulemavu watembelea Makumbusho ya Radio Vatican!

Baada ya Mkutano na Papa,ujumbe mawaziri walioshiriki katika Mkutano wa Watu wenye Ulemavu na Ujumuishi wa G7,uliofanyika huko Assisi na Perugia katika siku za hivi karibuni,walitembelea jumba la makumbusho ya kihistoria ya Baraza la utangazaji la kipapa katika jengo la Marconi.Ilikuwa ni wakati wa kusisitiza kwamba "mawasiliano lazima pia yawe katika huduma ya jamii jumuishi."

Vatican News

Wakati wa utamaduni, mshikamano na ushirikishwaji ilijionesha katika  Mawaziri wa G7 wa walemavu, baada ya kumaliza mkutano na Baba Mtakatifu  Francisko  walitembelea jengo la Marconi, katika bustani ya Vatican, nyumba ya makumbusho ya kihistoria ya Radio Vatican. Akiwakaribisha wajumbe walioongozwa na waziri wa ulemavu wa Italia, Alessandra Locatelli, Mwenyekti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini aliwataka mawaziri hao kuendelea kufanya kazi pamoja “kwa siku zijazo ambazo kila mtu, bila kujali uwezo wake, anaweza kuhisi kuwa sehemu muhimu ya jamii kwa sababu ni kwa njia hiyo tu tunaweza kutambua, hatua kwa hatua, ndoto ya jamii ambayo hakuna mtu anayetengwa inatimia.”

Mawaziri wa G7 wametembea makumbusho ya Radio Vatican.
Mawaziri wa G7 wametembea makumbusho ya Radio Vatican.

Dk. Ruffini alikumbusha kwamba, takriban miaka mia moja iliyopita baada ya kuzaliwa kwa Radio Vatican, kutokana na werevu wa Guglielmo Marconi, hata leo hii, Vatican linaweka teknolojia katika huduma ya mawasiliano inayoshinda kila aina ya vikwazo. Kwa hivyo alikumbuka mradi wa “Hakuna Mtu Aliyetengwa” na Programu ya “Vatican kwa wote” ambayo inalenga hasa kukuza mawasiliano ambayo yanajali wale walio pembezoni.

Mawaziri wa G7
Mawaziri wa G7

Ziara ya kutembelea makumbusho ya Radio Vatican iliambatana na kifungua kinywa kilichotolewa na Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) na kuandaliwa na vijana wa “Locanda dei Girasoli,” huduma ya upishi ambayo inachanganya umakini wa vyakula bora na ujumuishaji wa ajira kwa vijana walio na ugonjwa wa Utundio wa Ubongo, ugonjwa wa Williams na ulemavu mwingine wa utambuzi. Askofu Mkuu  Erio Castellucci, makamu  rais wa  Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na Sista Veronica Donatello, mkuu wa huduma ya kitaifa ya CEI kwa huduma ya kichungaji ya watu wenye ulemavu na mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambaye alishiriki katika kazi ya G7 huko Assisi na Solfagnano. Askofu Mkuu Castellucci na Sr Donatello waliwashukuru mawaziri kwa kujitolea kwao kuweka  kwa mara ya kwanza katika historia ya G7 - suala la ulemavu na ushirikishwaji katikati ya ajenda ya kimataifa.

Mawaziri wa G7 walitembelea makumbusho ya Radio Vatican.
17 October 2024, 12:07