Sinodi:Wajibu wa Mashemasi,kuanzishwa kwa ukristo&kusaidia maskini!

Katika muhtasari wa Oktoba 9,kuhusu kazi ya sinodi,Dk.Ruffini alisimulia uingiliaji kati wa mama mmoja na wasiwasi kwamba katika mkutano"hakuna mazungumzo ya kutosha kuhusu uanzishwaji tena wa ukristo kwa watoto wadogo."Kutoka Msumbiji,ombi kusaidia mateso ya watu na mafunzo ya mapadre.Ushuhuda wa shemasi wa kudumu:'kama hakuna njia ya sinodi,Kanisa halitaweza kuishi.'

Na Alessandro Di Bussolo na Angella Rwezaula – Vatican.

Ushuhuda ulioshangiliwa zaidi katika Ukumbi wa Paulo VI, kati ya meza za washiriki wa Sinodi ya Kisinodi inyaotendelea mjini Vatican, ulitoka kwa mama mmoja, mwenye wasiwasi mkubwa kwamba hakuna mazungumzo ya kutosha juu ya uanzishwaji tena wa ukristo kwa watoto wadogo, kiasi kwamba alitoa maombi kwa  msaada wa kuwalea watoto  katika imani ya Kikristo. Wanawake wanaendelea kuwa wahusika wakuu katika kazi na pia kumekuwa na wito wa kuwashirikisha zaidi katika majukumu ya kidiplomasia katika miktadha ya vita. Kwa upande wa Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na rais wa Tume ya Habari ya Sinodi, aliripoti hayo tarehe 9 Oktoba 2024  katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Chumba cha Wanahabari  mjini Vatican mchana. Akiwa na Sheila Pires, Katibu wa Tume hiyo hiyo, alitoa maelezo ya kazi ya makutaniko makuu ya tano na sita, yaliyofanyika tarehe 8  mchana na asubuhi ya tarehe 9 Oktoba ikiwa na  watu 343 walikuwepo katika ukumbi wa Mkutano huo wakati Papa Francisko alikuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro katika Katekesi yake ya kila juma.

Jukumu la lazima la walei katika Kanisa

Hatua hizo, zote zililenga mada ya utambuzi wa kikanisa, kwa hivyo mafunzo na vigezo, viwango tofauti vya uwajibikaji, jukumu la wahudumu waliowekwa rasmi." Kuhusu mada hiyo, Bi Pires alibainisha, kuwa kulikuwa na hotuba 35 za hiari tarehe 8 Oktoba  mchana na 21 asubuhi ya tarehe 9 Oktoba 2024. Kwa njia hiyo wajibu wa walei, ushirikiano wao na maaskofu na mapadre, ushiriki wao katika mchakato wa kufanya maamuzi, ilikuwa moja ya mada zilizojitokeza zaidi katika sehemu mbalimbali za mazungumzo kwa umma. “Umuhimu wa kuhimiza ushirikiano kati ya mapadre na walei ulisisitizwa na haja ya ushiriki mkubwa wa walei,  wanaume na wanawake katika majukumu ya uongozi,” alielezea Pires.

Hasa, ilitambuliwa kwamba uwepo wa walei ni wa lazima, wanashirikiana kwa faida ya Kanisa. Zaidi ya hayo, katika uingiliaji kati wa mmoja wao, pendekezo lilitolewa kushauriana na watu wa Mungu juu ya wale wanaofaa  katika ngazi ya ukuhani na uaskofu: "Askofu anaamua, lakini katika Kanisa la Sinodi ni Watu wa Mungu ambao wanapaswa kujisikia kuwajibika katika uchaguzi na pia kujua mahitaji ya wasifu wa kibinadamu na wa kiroho ambao wagombea wanapaswa kuwa nao.”

Wanawake na suala la kusikiliza

Katibu wa Tume ya Habari alielendelea kueleza kuwa “Pendekezo lingine lilihusu umuhimu wa kuweka tafakari ya kina juu ya nafasi ya walei katika zoezi la uchungaji katika parokia, kwa sababu mapadre wengi hawana wito wa kuwa mapadre wa Parokia, badala yake walei wengi kwa kuishi maisha ya ndoa yenye amani na maisha ya familia yanaweza pia kusaidia kutekeleza majukumu katika jamii." Bi Pires alifahamisha  kuwa “kuhusu wanawake ilipendekezwa kuepuka aina yoyote ya ubaguzi wa kijinsia katika ushirika, na hivyo kutambua zaidi mchango wao pia katika michakato ya kufanya maamuzi na kufikiria kusikiliza kama huduma ya wanawake wengi, inayosaidia ile ya paroko, shemasi na  katekista. Katika Ukumbi wa Mkutano walisema kuwa “Wanawake wanajua jinsi ya kusikiliza, wanasikiliza kwa njia tofauti na wangeweza kuifanya kama huduma, tofauti kabisa na kukiri. Pendekezo pia lilitolewa kuhusisha wanawake zaidi katika diplomasia katika ulimwengu uliogawanyika na wenye vita."

Kukabidhi vijana huduma ya kidijitali

Dk. Ruffini kisha alisisitiza kwamba washiriki katika Sinodi walionesha “haja ya kuungana na vizazi vipya kupitia uchungaji wa kidijitali.” Kisha mfano ulitolewa wa vijana wengi barani Afrika ambao wanakwenda Kanisani, kwamba wana talanta, nguvu na imani na kwa hiyo lazima wawe sehemu ya utambuzi wa kikanisa. Na ilipendekezwa kukabidhi huduma ya vijana kwa vijana: kwa ufupi ni vijana na sio watu wazima wafanye kama vijana, ili wajishughulishe na mazungumzo na wenzao walionaswa katika zama mpya au itikadi za kihuni,” alieleza Dk. Ruffini. Uingiliaji kati ulipendekeza tena hali ya kushangaza, ambapo watoto wengi ulimwenguni wanapitia hasa watoto wanaolazimishwa kuolewa wakiwa wachanga kwa sababu za kifamilia; wasichana waliolazimishwa kufanya ukahaba; waathirika wadogo wa biashara haramu ya binadamu." Na pia kulikuwa na mazungumzo ya "waseminari ambao wanatoka katika familia zisizo za Kikristo, au ambao wanalazimishwa kuingia kwenye ukuhani hata kama hawana wito kwa sababu ya heshima, au ya watu ambao wanapaswa kuficha hali yao ushoga wao."

Mama ahimiza uwajibikaji wa pamoja wa wazazi

Mkuu wa Baraza la Kipapa la mawasiliano alisisitiza kwamba "maneno ya Papa yalikumbukwa kwamba: Sinodi haina lengo la kutoa hati, lakini kuhamasisha vitendo. Kwa hiyo ilibainishwa tena kwamba haitatosha kusikiliza sauti za Kikristo tu na za parokia, bali kwa sauti za ujasiri zinazotoka nje, ili kuunda maeneo salama kwa watu kujitokeza." Na kisha alikumbuka ushuhuda wa mama mmoja  ambaye aliuliza  Mkutano huo unasema nini kuhusu jukumu la wazazi Wakristo, babu, na bibi katika kuchangia sinodi ya kusikiliza na utambuzi tangu utoto? Ni lazima tuwalee watoto wetu ili wanapokuwa wakubwa wamwendee Kristo." Kuhusu Hati ya mwisho, kwa hivyo, mwanamke aliomba kwamba, inapaswa kuhimiza majukumu ya uwajibikaji wa pamoja wa wazazi."

Kusindikiza waathiriwa wa unyanyasaji

Kwa njia hiyo marejeo yalifanywa kuhusu “haja ya kuwasindikiza waathrika wa nyanyaso  ndani ya Kanisa. Ilisisitizwa kwamba Kanisa lazima liwakaribie walio hatarini na kwamba nguvu lazima iwe huduma na kamwe sio ukasisi." Vivyo hivyo, Dk Ruffini aliripoti kuwa, "kulikuwa na ombi la kutoa umuhimu zaidi kwa maskini, pia katika mafunzo ya makuhani. Na zaidi hasa "maskini wako karibu na moyo wa Mungu, wana mamlaka na tunawaona kama suala la huduma na utume, lakini sio kama kuwaona wahudumu.” Katika Ulumbi wa Mkutano wa Sinodi, Dk. Ruffini aliendelea, "tulizungumza juu ya mapadre, hasa juu ya upweke wao, pia kwa sababu ya kazi nyingi. Kwa maana hiyo, ilisisitizwa kwamba umbali fulani wa mapadre hata katika sinodi unatokana na ukweli kwamba wengi wao wana mizigo inayowakabili, wanasimamia jumuiya mbalimbali na wana uzito mkubwa wa kiutawala". Sinodi iweze kufufua wito wao. "Kwa hiyo ilipendekezwa kutoa kila parokia ushauri wa kiuchumi na ikiwezekana pia miundo inayohusisha parokia kadhaa ili kuwasaidia mapadre wa parokia katika utumishi wao".

Tufikirie juu ya kucheza mechi na sio mazoezi

Zaidi ya hayo, kulikuwa na “mwaliko mkubwa wa mazungumzo, kati ya Makanisa na ndani ya Kanisa”. Na, Dk Ruffini aliripoti kuwa  "askofu wa China Giuseppe Yang aliingilia kati, kuleta salamu zake, na kusifu faida iliyoletwa na Mkataba wa 2018 kati ya Vatican  na China." Hatimaye, uingiliaji kati ulipendekeza kwamba mkutano uzingatie zaidi ukweli, pia katika utayarishaji wa hati ya mwisho. Kwa kutumia mfano wa mpira wa miguu, ilisemekana kwamba Kanisa, badala ya kucheza mechi, lijikite zaidi kwenye mazoezi.

Taarifa kutoka Kikundi cha Utafiti kuhusu Wanawake Kanisani

Dk. Ruffini aidha aliripoti kwamba mwishoni, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu  Kardinali Mario Grech alisoma taarifa kutoka kwa  Kardinali Víctor Manuel Fernández,  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, ambamo imebainishwa kuwa mada ya Kikundi cha Utafiti (Na. 5) kuhusu "Baadhi ya masuala ya kitaalimungu na kisheria kuhusu mitindo maalum za huduma (RdS 8 na 9)," hasa ushiriki wa wanawake katika maisha na uongozi wa Kanisa ambayo tayari yalikuwa yamekabidhiwa kwa Baraza hilo  kabla ya ombi la Sinodi. Kwa hiyo kazi hiyo lazima zifuate taratibu za Baraza lenyewe zilizowekwa katika kanuni zake, kwa kuzingatia uchapishaji wa Waraka maalum. Baada ya kuwasikiliza maaskofu na makadinali wa Feria IV, sasa iko katika awamu ya mashauriano: washauri tayari wanaotoa msingi wa hati. Ushauri huo pia unalenga wanawake ambao si washauri. Wanachama wote, wataalimungu wa kiume na wa kike wa Sinodi wanaweza kutuma maoni na mapendekezo katika miezi ijayo. Tarehe 18 Oktoba 2024 wataalimungu wawili wako tayari kupokea mapendekezo juu ya mada hiyo kwa maandishi au kwa mdomo.

Hotuba za wageni watatu katika Ofisi ya Vyombo vya habari

Baada ya Mhutasari wa Sinodi inayoendelea ilifuata kipengele kingine cha wageni waliosindikiza mkutano na waandishi. Kwa njia hiyo wajibu wa mashemasi wa kudumu katika Kanisa na ushiriki wao katika Sinodi, uanzishwaji wa Kikristo na kutelekezwa kwa jumuiya na vijana na hali ya kiroho ya sinodi inayoongoza kwa "utakaso" wa mahusiano ya kibinadamu katika Kanisa na jamii; lakini pia ombi la msaada kutoka kwa Kanisa nchini Msumbiji, ndizo mada zilizoguswa na wageni hao watatu katika Ofisi ya Habari ya Vatican, wawakilishi wa mabara matatu, kutoka bara la Afrika, Amerika na Ulaya. Maswali yaliyoulizwa zaidi na waandishi wa habari, baada ya hotuba yake ya kwanza, alikuwa Shemasi Geert De Cubber, shahidi wa mchakato wa sinodi, Mtaalimungu, mwandishi wa habari wa zamani, shemasi wa kudumu wa Jimbo la  Ghent (Ubelgiji) na mjumbe wa kiaskofu wa katekesi na huduma ya vijana na anayefahamika. Ni mjumbe pekee wa Baraza hilo ambaye ni shemasi wa kudumu, aliyeoa, mwenye watoto katika  Kanisa la Kilatini, ingawa kutoka Makanisa Katoliki ya Mashariki pia kuna mmoja kutoka Kanisa la Siria na Melkite, ambaye hivi karibuni atapewa daraja la upadre.

Shemasi wa kudumu De Cubber: mkutano wa baada ya sinodi kwa mashemasi

Shemasi De Cubber alirudia yale yaliyosemwa tayari katika ukumbi wa Sinodi kwamba " shemasi ni mjenzi wa daraja katika familia ("na mimi” ) alibaninisha: "Nilifanya maandalizi kabla ya Sinodi na mke wangu na watoto watatu, ili niweze kuwa hapa") pamoja na familia zingine, katika jamii na pia na jamii ya nje, na hii inaweza kuwa muhimu sana katika jumuiya isiyo ya kidini kama ile ya Ubelgiji, ambayo Papa aliitembelea mwishoni mwa Septemba baada ya Luxembourg.  Shemasi huyo liongeza kuwa kazi ya shemasi ni kutoka na “kwenda mahali ambapo Kanisa haliendi, kwa wale ambao hawana sauti na wametengwa na Kanisa lenyewe na jamii na kuwarudisha ndani ya Kanisa.” Katika Kanisa ambalo watendaji mara nyingi wamechoka na wazee na pale ambapo “tusipokwenda kwa njia ya sinodi Kanisa halitaweza kuendelea kuishi”, shemasi wa Ubelgiji alijaribu kuleta sinodi miongoni mwa vijana, akiunganisha katika juhudi huduma za vijana za majimbo yote yanayozungumza Kiflemish. "Wakati huo huo tumebadilisha jina letu, sasa sisi ni 'Kammino', na 'K' ikionesha kuwa Wakatoliki, katika lugha yetu." Akichochewa na swali kutoka kwa mwandishi wa habari, alikiri kwamba mashemasi wangeweza kuwakilishwa vyema zaidi katika Sinodi, na kwamba anajua kwamba kuhusu hili mashemasi huko Marekani, "ambapo huduma ina nguvu sana, hawafurahii sana, ukweli kwamba sisi ni wachache."  Hivyo alipendekeza mkutano wa baada ya sinodi wa mashemasi katika siku zijazo, kama ilivyokuwa mwaka huu na mapadre wa parokia. "Kuwa shemasi sio kwangu kabisa maandalizi ya ukuhani, sina wito huo. Lakini yetu ni huduma ya huduma ya kipekee," alihitimisha De Cubber -

Chile na utajiri wa Ushemasi wa kudumu

Alipoulizwa juu ya mada hiyo, Askofu mkuu wa Puerto Montt (Chile),Askofu Mkuu  Luis Fernando Ramos Pérez, alisisitiza kwamba katika nchi yake, baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatikani, mashemasi wengi wa kudumu waliwekwa wakfu, leo hii "kuna zaidi ya makuhani na wataw na mchango wao "ni wa ajabu na wa kuthaminiwa, wanasimamia parokia na paroko.” Lakini wao si “makuhani wadogo.” Kwa upande wake, Askofu Mkuu  Inácio Saure, wa Jimbo Kuu la Nampula, rais wa Baraza la Maaskofu wa Msumbiji, na mwanashiriki wa  Wamisionari wa Consolata, alieleza kwamba kwa sasa hakuna mashemasi wa Kudumu katika Kanisa lake, "kwa sababu tumejitolea sana kwa mafunzo ya makuhani" hata ikiwa katika siku zijazo, ikiwa kuna uwezekano, bila shaka watawekwa wakfu. Pia kuandaa jumuiya za parokia, ambao shemasi wa kudumu  anapofika, wanatuuliza mara moja: 'Kwa nini hasherehekei?'

Msumbiji bado inahitaji msaada

Askofu Mkuu wa Afrika, akijibu swali, huku akialika Sinodi kujulisha hali ya kushangaza ya nchi yake, iliyoharibiwa na vita vilivyoanza mwaka 2017 (sasa vimesimamishwa) na vifo vya elfu 5 na watu milioni moja waliokimbia makazi. Hata kama msaada mwingi umefika huko nyuma “Watu wa leo wanateseka sana, na wameachwa peke yao. Kwa hiyo zaidi inaweza kufanyika”, kwa kubadilishana zawadi za kimwili “kati ya Makanisa ambayo yana mengi na yale yaliyo katika umaskini”. Katika hotuba yake, Askofu Mkuu Saure aligusia mada ya umuhimu wa kuanzishwa kwa ukristo kuwa ni kukutana kibinafsi na Kristo, akionesha kwamba “hata hapa vijana wanahama kutoka Kanisani baada ya kupata kipaimara”, kwa hiyo inapaswa kutiliwa maanani zaidi. Alieleza kuwa katika miaka sita iliyopita, akishughulika na huduma ya vijana, amejaribu kuifanya "na vijana, kwa vijana na kwa vijana" na kwamba kutangazwa kuwa mtakatifu wakati wa Sinodi Mwanzilishi wa Shirika lake kunaweza pia kuleta kichocheo. Hii ni kwamba  Oktoba 20 2024  Mwanzilishi wa Wamisionari wa Consolata, Mwenyeheri Allamano, ambaye alisema "watakatifu wa kwanza kisha wamisionari", ningesema, "watakatifu wa kwanza na kisha Wakristo."

Pérez: kusafisha uhusiano katika Kanisa na na jamii

Askofu Mkuu Ramos Pérez alizungumzia hali ya kiroho ya sinodi ambayo inabadilisha miundo ya Kanisa katika hotuba yake, akiripoti kwamba katika Sinodi kulikuwa na mazungumzo ya "hali ya kiroho ya kibinafsi ambayo inasukuma kuelekea wongofu wa kichungaji wa mtu binafsi na wa jumuiya."Ili hatimaye kufikia "utakaso" wa mahusiano ya kibinadamu katika Kanisa na na jamii, kwa sababu leo ​​baadhi ya mahusiano husababisha ukuaji na wengine "wanaweza kuharibu". Njia ni kuishi upendo kwa kuchukua mfano kutoka kwa Kristo. Na alimalizia kwa kusisitiza kwamba wale walio na majukumu katika Kanisa lazima wayatekeleze kwa “vigezo vya sinodi, kufanya maamuzi” kwa kushauriana na msingi. Katika hili “utambuzi wa sinodi unahitajika, ambao pia unahusisha walei wanaume na wanawake, si wahudumu waliowekwa rasmi tu”.

Kikao 5 na 6 cha Sinodi 9 Oktoba 2024
10 October 2024, 09:46