Papa akutana na Makamu rais wa Bolivia
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko alikutana katika Jumba la Kitume, Alhamisi tarehe 29 Novemba 2024 na Makamu wa Rais wa Bolivia David Choquehuanca Céspedes. Baadaye, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican, Bwana Choquehuanca Céspedes alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mahojiano katika Sekretarieti ya Nchi
Kwa mujibu wa taarifa inasomeka kuwa “Wakati wa majadiliano mazuri katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mzuri kati ya Vatican, Bolivia na Kanisa mahalia ulisisitizwa na mchango wa mwisho kwa jamii ya Bolivia ulizingatiwa.” Zaidi ya hayo, wakati wa mazungumzo “hawakukosa kujikita na baadhi ya vipengele vya hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini Bolivia.”
Kushiriki katika semina huko Jumba la Mtakatifu Calist
Bwana Choquehuanca Céspedes alishiriki tarehe 28 Novemba 2024 katika semina Kwenye Jumba la Mtakatifu Calisiti kuhusu “kushughulikia matatizo ya mgogoro wa mazingira katika nuru ya Waraka wa Laudato si' na Laudate Deum, uzoefu katika Amerika ya Kusini,” iliyandaliwa na Ubalozi za Bolivia, Cuba na Venezuela wanawakilisha nchi zao mjini Vatican kwa ushirikiano na Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini. Katika hotuba yake, makamu wa rais alishutumu “ubepari wa kijani, sababu ya mgogoro uliovuka ambao unaathiri hasa wakazi wa kiasilia, na pia wasomi wa nchi ambazo, kwa kutumia maendeleo ya uhandisi, huzalisha kile tunachokiona leo hii: vita, njaa.”