Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
PROGRAMU YA KISWAHILI
Ratiba Podcast
Papa Francisko wakati wa sala kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Amani huko Hiroshima mnamo 2019(Vatican Media). Papa Francisko wakati wa sala kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Amani huko Hiroshima mnamo 2019(Vatican Media).  (Vatican Media) Tahariri

Silaha tena na 'mwavuli wa nyuklia'-maneno ya Papa Francisko!

Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Dk.Andrea Tornielli,anaandika tahariri yake kuhusu suala la kujihami kwa silaha barani Ulaya akikumbusha maneno ya kinabii ya Papa Francisko:'Tunawezaje kupendekeza amani ikiwa mara kwa mara tunaomba tishio la vita vya nyuklia kama njia halali ya kusuluhisha mizozo?'

Na  Andrea Tornielli

Upepo wa vita, uwekaji silaha mpya unaohusisha uwekezaji mkubwa, mapendekezo ya kufufua silaha za nyuklia… Inashangaza sana Ulaya na ulimwenguni kote, jinsi ambavyo mashindano ya silaha yanawasilishwa kama matarajio yasiyoepukika, muhimu na kama ndiyo njia pekee ya kuchukua. Baada ya miaka mingi ya ukimya kuanzia na diplomasiana kutokuwepo kwa uwezo wa mazungumzo, inaonekana kwamba njia pekee inayowezekana ni kuweka silaha tena. Mababa waanzilishi (wa Umoja wa Ulaya), kama vile Alcide De Gasperi, ambaye aliunga mkono kuundwa kwa jeshi la pamoja la Ulaya, wanaombwa kuhalalisha mipango tofauti sana, ambayo haihusishi Umoja wa Ulaya lakini mataifa binafsi. Tunazungumza tena juu ya "mwavuli wa nyuklia" na "kuzuia," ambayo hufufua hali mbaya zaidi za Vita Baridi, lakini katika hali ya kutokuwa na utulivu na kutokuwa na uhakika ikilinganishwa na karne iliyopita na dimbwi la Vita vya Kidunia vya Tatu vilivyo karibu zaidi.

Katika miaka ya hivi karibuni, kwa uwazi wa kinabii, Papa Francisko ameona hatari inakaribia. Maneno yake yanaakisi katika kuelewa wakati tunaoishi. Kwa njia hiyo tunakuza sauti ya Papa, wakati amelazwa katika Hospitali ya Gemelli,  Roma, akitoa mateso yake na sala za amani duniani. Papa Francisko kunako  Novemba2017 alisema: "Kweli Kupanda kwa mbio za silaha kunaendelea bila kupunguzwa na bei ya kisasa na kutengeneza silaha, sio silaha za nyuklia tu, bali zinawakilisha gharama kubwa kwa mataifa. Matokeo yake, vipaumbele halisi vinavyoikabili familia yetu ya kibinadamu, kama vile vita dhidi ya umaskini, kukuza amani, kutekeleza mipango ya elimu, ikolojia na huduma za afya na maendeleo ya haki za binadamu, yamewekwa katika nafasi ya pili ... silaha zinazosababisha uharibifu wa Jumuiya ya binadamu hazina maana hata kwa mtazamo wa kimbinu..."

Kunako Novemba 2019, akiwa  Nagasaki, jiji lile lililouawa kishahidi kwa bomu la atomiki, Askofu wa Roma alisema: "Moja ya matamanio ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu ni usalama, amani na utulivu. Umiliki wa silaha za nyuklia na maangamizi makubwa sio jibu la shauku hii; kwa hakika inaonekana daima kuizuia. Ulimwengu wetu umeakisiwa na mgawanyiko potovu ambao unajaribu kutetea na kuhakikisha utulivu na amani kupitia hisia potofu ya usalama inayodumishwa na mawazo ya woga na kutoaminiana, ambayo mwishowe hutia sumu uhusiano kati ya watu na kuzuia aina yoyote ya mazungumzo." Aliongeza, "Amani na utulivu wa kimataifa haviendani na majaribio ya kujenga juu ya hofu ya uharibifu wa pande zote au tishio la maangamizi kamili. Inaweza kufikiwa tu kwa msingi wa maadili ya kimataifa ya mshikamano na ushirikiano katika huduma ya siku zijazo inayoundwa na kutegemeana na uwajibikaji wa pamoja katika familia nzima ya binadamu ya leo na kesho."

Pia mnamo Novemba 2019, huko Hiroshima, Papa Francisko alikumbuka, akikubali maneno ya Papa Paulo VI, kwamba amani ya kweli inawezekana tu bila silaha: "Kiukweli, ikiwa tunataka kujenga jamii yenye haki zaidi na salama, lazima tuache silaha zianguke kutoka mikononi mwetu.  “Hakuna awezaye kupenda akiwa na silaha za kukera mikononi mwake”(Mtakatifu Paulo VI akihutubia UN( United Nations Address tarehe  4 Oktoba 1965, 10). Tunapokubali mantiki ya silaha na kujitenga na mazoezi ya mazungumzo, tunasahau hasara kwamba, hata kabla ya kusababisha waathirika na uharibifu, silaha zinaweza kuunda jinamizi; "zinahitaji gharama kubwa, kukatiza miradi ya mshikamano na kazi muhimu, na kupotosha mtazamo wa mataifa" (ibid.)  Je, tunawezaje kupendekeza amani ikiwa daima tunaomba tishio la vita vya nyuklia kama njia halali ya kutatua migogoro? Shimo la uchungu linalovumiliwa hapa litukumbushe mipaka ambayo haipaswi kuvuka. Amani ya kweli inawezekana tu kuwa amani isiyo na silaha."

Sauti ya Mrithi wa Petro, aliendelea, ni “kuwa sauti ya wasio na sauti, wanaoshuhudia kwa wasiwasi na uchungu mivutano inayokua ya wakati wetu,  ukosefu wa usawa usiokubalika na ukosefu wa haki ambao unatishia kuishi pamoja kwa binadamu, kutokuwa na uwezo mkubwa wa kutunza nyumba yetu ya pamoja, na kuzuka mara kwa mara kwa vita vya kutumia silaha, kana kwamba haya yanaweza kuhakikisha mustakabali wa amani." Kisha alilaani sio tu utumiaji bali pia umiliki wa silaha za nyuklia, ambazo bado zinajaza ghala la ulimwengu na nguvu inayoweza kuharibu ubinadamu mara nyingi: "Kwa imani kubwa ningependa kutangaza tena kwamba matumizi ya nishati ya atomiki kwa madhumuni ya vita ni leo hii, zaidi ya hapo awali, uhalifu sio tu dhidi ya hadhi ya wanadamu lakini dhidi ya mustakabali wowote unaowezekana kwa nyumba yetu ya pamoja. Matumizi ya nishati ya atomiki kwa madhumuni ya vita ni kinyume cha maadili, kama vile kuwa na silaha za nyuklia ni kinyume cha maadili, kama nilivyosema miaka miwili iliyopita. Tutahukumiwa kwa hili."


Kulingana na Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani, lililotajwa na gazeti la kila siku la Italia lililochapishwa Ulaya, kuna vichwa 290 vya nyuklia chini ya udhibiti wa Ufaransa na vichwa 225 Nchini Uingereza. Idadi kubwa ya vichwa vya nyuklia - 88% - viko kwenye ghala za silaha za Marekani na Urusi, vikiwa na zaidi ya vichwa 5,000 kwa kila moja. Kwa ujumla, nchi tisa zinamiliki mabomu ya nyuklia, zikiwemo China, India, Korea Kaskazini, Pakistan na Israel. Leo, kuna makombora ya balestiki yenye uwezo wa kufyatua nguvu za uharibifu mara elfu zaidi ya mabomu yaliyodondoshwa huko Hiroshima na Nagasaki mnamo 1945. Mtu anaweza kujiuliza: je, tunahitaji silaha zaidi? Je, hii ndiyo njia pekee ya kujitetea?

"Kanisa Katoliki," Papa Francisko alisema huko  Nagasaki miaka sita iliyopita, "limejitolea bila kubatilishwa kukuza amani kati ya watu na mataifa.  Huu ni wajibu ambao Kanisa linahisi kuwa limefungwa mbele ya Mungu na kila mwanamume na mwanamke katika ulimwengu wetu... Kwa kuwa nina hakika kwamba ulimwengu usio na silaha za nyuklia unawezekana na ni muhimu, ninawaomba viongozi wa kisiasa wasisahau kwamba silaha hizi haziwezi kutulinda kutokana na vitisho vya sasa vya usalama wa kitaifa na kimataifa."

Tahariri ya Dk.Tornielli
16 Machi 2025, 15:06
Prev
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031     
Next
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930