Tafuta

G20 Jukwaa la Bali nchini Indonesia G20 Jukwaa la Bali nchini Indonesia 

B20 nchini Indonesia nafasi ya dini katika kuzindua majadiliano kati ya Wakuu wa Mataifa

Mkutano wa XVII wa Wakuu wa Nchi na Serikali unafanyika huko Bali, Indonesia kuanzisha 15-16 Novemba.Miongoni mwa mada zilizopo katikati ni amani,ulinzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.Mkutano wa nchi ya Marekani na China umefanyika.Wawakilishi wa harakati,vyama na viongozi wa kidini katika majadiliano kwa manufaa ya wote na maelewano ya watu wapo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mkutano wa XVII wa B20, ambao ni jukwaa la wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu ulioundwa tangu mwaka 1999 baada ya mfululizo wa migogoro ya kifedha, umeanza tarehe 15 na 16 Novemba 2022 huko Bali, Indonesia, ili kupendelea kimataifa uchumi kwa kuzingatia uchumi mpya unaoendelea. Umoja wa  nchi za Ulaya na nchi 19 zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani zinashiriki, kama vile Saudi Arabia, Argentina, Australia, Brazil, Kanada, China, Korea Kusini, India, Indonesia, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Mexico, Uingereza, Urussi, Marekani, Afrika Kusini na Uturuki. Miongoni mwa mada za mkutano huo, ni mzozo wa chakula, mvutano kuhusu nishati, vita vya Ukraine na matokeo yake  duniani, ongezeko la mfumuko wa bei na hatari ya mdororo wa uchumi duniani kwa madhara kwa nchi maskini zaidi.

Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia
Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia

Migawanyiko kati ya Mashariki na Magharibu ya dunia inashika kasi

Katika hali ambayo migawanyiko kati ya Mashariki na Magharibi ya dunia inazidi kushika kasi, huku China na Urusis zikiwa upande mmoja na Marekani na Ulaya kwa upande mwingine nazo pia ziko kwenye B20 huko Bali, kwa mujibu wa  Padre Marcin Schmidt, Padri mmisionari kutoka Poland na mtaalam wa mambo ya mgogoro  kwamba "kuna matarajio makubwa ya mkutano unaowezekana kati ya wajumbe wa Urussi na Ukraine, na ule kati ya wajumbe wa Urussi na Amerika na kawaida, kuna maandalizi makubwa pia kuhusu usalama. Sehemu ya jiji la Bali kwa sasa  inahisi kama ngome." Huko watakutana na wawakilishi wengi wa nchi nyingine nyingi na pia wa vyama na harakati kwa sababu kati ya mada  hizo kuna si tu matarajio, juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa rais wa Kirussi au Kiukreni, lakini Indonesia akiwa ni  rais wa sasa wa B20 kwa mwaka 2022, alifafanua wazi jinsi katikati ya mkutano huo kuna uwezo, baada ya Uviko -19, kurejesha uwezekano wa kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wote kuanzia mabadiliko yanayotokea katika ulimwengu wa kisasa", alisisitiza Padre Schmidt.

Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia
Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia

Scholas Occurrentes huko Bali

Miongoni mwa harakati za kimataifa zilizopo  huko Bali pia kuna  Scholas Occurrentes ambao wanashiriki katika mikutano juu ya mada ya elimu. Vijana ni mojawapo ya vipaumbele vya B20, kwa ajili ya majadiliano kati ya vizazi na uwepo wao katika ulimwengu wa kidijitali. Kwa mfano, moja ya majopo ya B20 itahusu ulinzi wa haki za watoto katika ulimwengu wa kidijitali, kutokana na mtazamo wa kisheria na kwa sababu ufikiaji wa mtandao ni wa haki na haki kwa vijana wanaoishi katika nchi zilizo maskini zaidi.

Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia
Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia

Majadiliano ya kidini

Kwa mujibu wa padre Schmidt alithibitishwa kwamba anaamini kuwa majadiliano  ya kidini kidini katika B20 ya Indonesia yanaweza kuwa na jukumu muhimu, pia kwa sababu wako katika nchi, Indonesia ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa kilele   cha mwaka huu, ambayo kwa ishara yake, katika kauli mbiu yake kuu, isemayo 'Tumeungana katika tofauti'. Majadiliano ya kidini yatakuwa mhusika mkuu katika mikutano mingi huko Bali kwa lengo la kudumisha na kuimarisha uwiano na ushirikiano kati ya viongozi dunia ya kidini hasa kwa ajili ya amani. Kwa mara ya kwanza, kiukweli, mkutano huo unatoa nafasi kwa dini na mchango wao katika maendeleo shirikishi ya mwanadamu na utamaduni wa amani." Ndio maana ilianzishwa ya 'Breligioni 20' ambayo inajumuisha, pamoja na mambo mengine, mkutano kati ya vijana wa dini mbalimbali ili kuzungumzia mchango ambao vizazi vipya na imani za kidini zenyewe zinaweza kutoa katika maendeleo shirikishi ya binadamu. Kwa kutambua umuhimu wa kujumuisha ushirikiano kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea ni muhimu sana na katika hali hii dini zinaweza kufanya mengi kwa majadiliano  yao kusaidia kujenga utamaduni wa kukutana, utamaduni wa mazungumzo na ushirikiano,” alihitimisha.

Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia
Wakuu wa Mataifa katika Jukwaa la G20 huko Bali nchini Indonesia

Mada kuu

Umakini ambao sio tu kwa wakuu wa nchi lakini kuna  mada ya mpito wa nishati, mada msingi kama amani na uchumu, katika urais wa Indonesia wa B20. Mpito ambao lazima uwe wa haki na wa kuunga mkono. Katika ajenda, hata kama si moja kwa moja, kuna mada nyingi ambazo ni sehemu ya Majisterio ya Papa. Hasa, "Uchumi wa Francesco". Katika moja ya matukio kando ya mkutano wa kilele wa B20 kuna majadiliano  ya haja ya kuunda uchumi mpya, jumuishi, kwa mfano ulioainishwa huko Assisi. Na ni muhimu kwamba B20 ichunguze maono mapya ya kiuchumi kuanzia pendekezo la Papa. Kwa hakika, huko Bali, mijadala mbalimbali ya kundi la B20 yanajaribu kupendekeza falsafa, mfano wa Indonesia, ambayo inazungumzia maelewano katika uhusiano na wat, wenyewe binafasi, kuanzia katika maelewano na Mungu na asili.

Indonesia
15 November 2022, 12:00