Nicaragua yafuta hadhi ya kisheria ya NGO 16 na baadhi ni ya Kikristo
Vatican News
Serikali ya Nicaragua Jumanne tarehe 16 Januari 2024 ilifuta hadhi ya kisheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali 16 (NGOs)ambamo miongoni mwake ni ya Kikatoliki na kiinjili. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, mashirika tisa yasiyo ya kiserikali yamefungiwa kwa kushindwa kufuata kanuni zinazowaongoza na kukwamisha shughuli za uangalizi na ufuatiliaji zinazotolewa na mamlaka.
Mali ya Mashirika ya Kikristo inahamishiwa serikalini
Mali inayohamishika na isiyohamishika ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGOs)kwa njia hiyo itahamishiwa Serikalini. Mashirika mengine yasiyo ya kiserikali 7 hata hivyo, yamewasilisha maombi kwa hiari ya kuvunjwa. Zaidi ya mashirika 3,500 yasiyo ya kiserikali yamevunjwa na serikali huko Managua tangu 2018, mwaka ambapo maandamano ya wananchiya kupinga mageuzi ya hifadhi ya jamii yalipozuka.