Zanzibar,Tanzania:Shindano la Kimataifa la Kitesurf 2024,Kiwengwa Februari 10
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akikazia kusema kuwa : “Kukuza mchezo ambao ni kwa ajili ya kila mtu, mshikamano unaoweza kufikiwa na kulengwa kwa kila mwanamume na mwanamke ni dhamira kubwa na changamoto ambayo hakuna mtu anayeweza kuifanya peke yake. Kiukweli, kwa kucheza tu kama timu na kuwa pamoja inawezekana kufikia malengo ya kauli mbiu ya Olimpiki: altius, citius, fortius, yaani: juu zaidi, haraka zaidi na ngumu zaidi. Baba Mtakatifu alisisitiza hayo wakati wa kutoa hotuba yake kwa Washiriki wa Kongamo la Kimataifa la Michezo mnamo tarehe 30 Septemba 2022, lililokuwa limeandaliwa na Baraza la Walei, Familia na Maisha.
Ni Katika Mkatadha wa mchezo ambapo mnamo tarehe 10 Februari 2024 limethibitishwa tena shindano la Kimataifa ambalo liliahirishwa kutokana na kukosekana kwa upepo ambalo lingefanyika mnamo tarehe 27 Januari 2024, la Kitesurf, katika Fukwe za Kiwengwa huko Zanzibar, lililoandaliwa na Shirika lisilo la kibishara, Baraza la Michezo la Taifa Zanzibar(ZNSC)na Kamati ya Kiwengwa Kitesurf (KKC),ambayo inawakilishwa na shule mbili za zanzibar za kitesurf: Onelove Kite na Jambo Kite. Mashindano haya ya kimataifa yameidhinishwa na Serikali ya Zanzibar na Wizara ya Utalii, Jumuiya ya Hoteli Zanzibar, Ubalozi wa Tanzania nchini Italia na Ubalozi wa Italia nchini Tanzania. Shindano hili litawaona watu 20 kutoka mataifa mbali mbali 9 kwa lengo la kuwa pamoja na kusheherekea msimu wa kwanza wa mchezo huo wa Kitesurf 2024.
Mchezo wa Kitesurf katika fukwe za Kiwengwa, umri 17-77
Muandaaji mkuu Daktari Stefano Conte, na ambaye ni Daktari wa Watoto, kama mpenda mchezo huo, alifanya juhudi kubwa ya maadalizi kutokana na uzoefu wake ili kuunganisha watu wa mataifa mbali mbali kufanya uzoefu huo wa pamoja, kwa mara ya kwanza katika eneo hilo la Zanzibar. Kwa njia hiyo katika muktadha huu tena Dk Conte anawaalika wote kushiriki ili kuona mchezo huo kabambe wa mashindano ambao unajumuisha vijana kuanzia umri wa miaka 17 hadi 77 wote wanaalikwa kujionea na ni matumaini yake watafika wengi na kuupenda mchezo huo pamoja na ushindi. Ikumbukwe kuwa mchezo huo umehamasishwa na Shirika lisilo la kiserikali na hivyo siyo wa kibiashara.