Tafuta

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 670 wanahofiwa kufariki baada ya maporomoko ya ardhi ya Papua New Guinea Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 670 wanahofiwa kufariki baada ya maporomoko ya ardhi ya Papua New Guinea  (ANSA)

Papua New Guinea:Zaidi ya 40% ya waliokumbwa na maporoko ni chini ya miaka 16

Juhudi zinaendelea za utafutaji na uokoaji zinaongozwa na Kikosi cha Ulinzi cha Papua New Guinea katika hali ngumu sana,huku ardhi ikiwa bado haijatengemaa na barabara kuharibika na hivyo kuzuia ufikiaji wa eneo la maafa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia watoto(UNICEF) linaongeza hatua yake ya dharura kufuatia maafa ya Ijumaa tarehe 24 Mei  iliyopita katika jimbo la Enga, nchini Papua New Guinea, na kusababisha vifo vya mamia ya watu, kuharibu miundombinu muhimu na kuwaacha maelfu bila makazi. Hata sasa Juhudi zinaendelea za utafutaji na uokoaji zinaongozwa na Kikosi cha Ulinzi cha Papua New Guinea katika hali ngumu sana, huku ardhi ikiwa bado haijatengemaa na barabara kuharibika, na hivyo kuzuia ufikiaji wa eneo la maafa.

Misaada inapelekwa huko Paua New Guinea kusaidia watu
Misaada inapelekwa huko Paua New Guinea kusaidia watu

“Tunafanya kazi kwa karibu na mamlaka na mashirika ya jamii nchini Papua New Guinea kutoa msaada muhimu kwa waathirika wa janga hili baya,” alisema hayo Angela Kearney, Mwakilishi wa UNICEF. Sasa ni wazi kuwa zaidi ya 40% ya walioathiriwa ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 16, walioumizwa sana na kupoteza familia zao, nyumba na njia za kujikimu.”

Watu zaidi ya 600 wamefunikwa na maporomoko
Watu zaidi ya 600 wamefunikwa na maporomoko

Katika majibu ya awali, ya UNICEF ilisambaza vifaa vya usafi vilivyokuwa na ndoo, makopo ya jeri na sabuni, pamoja na leso zinazoweza kutumika tena, wipes za matumizi mbalimbali na vitu vingine ambavyo vilikuwa vimewekwa awali na Mamlaka ya Afya ya Mkoa.

Maporomoko Papua Guine yalifunika watu zaidi ya 600
Maporomoko Papua Guine yalifunika watu zaidi ya 600

UNICEF ilishiriki katika tathmini za haraka ili kubaini mahitaji mapana ya maji, usafi wa mazingira, elimu, ulinzi wa watoto, afya na lishe kwa jamii zilizoathirika. Wakati huo huo, vituo vya uokoaji, vinavyoungwa mkono na mamlaka mahalia  na Jeshi la Ulinzi la Papua New Guinea, vinatoa huduma muhimu na msaada kwa watu waliohamishwa.

Maporomoko makali huko Papua New Guinea
Maporomoko makali huko Papua New Guinea
Msaada wa UNICEF kwa Papua New Guinea
29 May 2024, 11:10