Algeria:Tebboune athibitishwa tena kuwa rais
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Takriban 95% ya wapiga kura walitoa maoni yao kumuunga mkono Abdelmadjid Tebboune ambaye kwa hiyo anafanikiwa kuongoza tena Algeria. Kwa hiyo ni kura ambayo kwa kiasi kikubwa inathibitisha utabiri wa matumaini zaidi. Hakuna cha ushindi wa Abdelali Hassani, mgombea wa Kiislamu, ambaye wafshabiki wake wanashutumu udukuzi wa kura na mwanasoshalisti Youssef Aouchiche, ambaye kati yao alipata zaidi ya 5% tu ya kura.
Nusu ya Algeria haikupiga kura
Dosari pekee katika uchaguzi huo wa mapema, kwa mujibu wa waangalizi, ni kutokuwepo kwa kiasi kikubwa cha kwenda kufanya uchaguzi wa zaidi ya nusu ya Waalgeria, takwimu ambayo bado ni bora kuliko uchaguzi wa 2019, ambapo karibu 40% ya wale walio na haki ya kupiga kura walipiga kura. Kuna wanaozungumzia kususia kupiga kura baada ya vuguvugu maarufu la Hirak, lililosaidia kuuangusha utawala wa rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika, na kutengwa.
Kuboresha muundo wa kijamii na kiuchumi
Rais Tebboune, anayeshutumiwa kwa kutumia sera ngumu na upinzani, sasa ataendelea kutekeleza mpango wa kuboresha hali ya uchumi ya nchi ya Algeria, ambayo hutoa gesi na hidrokaboni kwa nusu ya Ulaya, hata hivyo atakosa umaarufu wa uungwaji mkono unaotarajiwa na chama chake, “National Liberation Front), hasa kwa sababu ya msimamo mkali wa kutoshiriki.