Mtazamo wa Ulimwengu wetu
Na Angella Rwezaula - Vatican
Kwa mtazamo wa kinachoendelea Ulimwenguni tunaweza kuona mengi tu kwa kudadavua lakini kwa ufupi tuanzie na sehemu zile ambazo vyombo vya habari vinamulika zaidi: Marekani: matokeo ya kwanza baada ya "siku ya uchaguzi": Donald Trump yuko mbele, na ameshinda katika majimbo 2 ya (Georgia na Caroline Kaskazini), ushindi mwekundu pia huko Pennsylvania. Warepublican wanachukua viti vingi katika Seneti. Ni matokeo ambayo hayana uhakika lakini nafasi za Kamala Haris zimepunguzwa. Wakati Israel: Netanyahu amfuta kazi Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant na kumweka Israel Katz, baada ya kutofautiana kuhusu vita huko Gaza. Giedon Saar, mpinzani wa zamani wa waziri mkuu, anachukua nafasi ya Mambo ya Nje.
Lebanon: Watu 15 walikufa tarehe 5 Novemba 2024 katika shambulio la Israeli kwenye jengo la makazi huko Barja kusini mwa Beirut na - Urusi: Baraza la Shirikisho (Jumba la Juu) linapiga kura tarehe 6 Novemba 2024 kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kimkakati na Korea Kaskazini. Kwa upande wa Ukraine: mji wa Zaporijgia ulipigwa tarehe 5 Novemba na watu 6 walikufa wakati watu 23 kujeruhiwa. Kwa mtazamo wa Congo- DRC: Wanajeshi wanne walihukumiwa kifo kwa kupora parokia moja. Na - Italia: Rais Mattarella akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Antonio Tajani wanazuru nchini China hadi tarehe 12 Novemba 2024.